Kili Marathon yaleta msisimko Moshi
Mwandishi Wetu
MJI wa Moshi tayari umepata msisimko
mkubwa huu watu wakianza kufurika kufuatia mbio za Kilimanjaro Marathon 2017
ambazo zinatarajiwa kufanyika Jumapili Februari 26.
Tayari hoteli, nyumba za kulala
wageni na sehemu nyingine zinazotoa huduma mbalimbali zimeonekana kuwa na watu
wengi kuashiria mambo yameiva huku zoezi la kujisajili likifikia tamati
Jumamosi saa sita mchana.
“Kwa kweli msisimko uliopo Moshi
sasa hizi ni wa aina yake na ndio maana sisi tukiwa wadhamini wakuu tunapata
nguvu ya kuendelea kudhamini mbio hizi kwani ni kubwa na huwaleta watu wengi
pamoja,” alisema Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager Pamela Kikuli
ambaye bia yake ndio mdhamini mkuu wa mbio hizo.
“Mbio za mwaka huu zinatarajiwa kuwa
kubwa zaidi na ni matumaini yetu kuwa watu watajitokeza kwa wingi. Tumejiandaa
vizrikabisa kwani baada yam bio kutakuwa na burudani kutoka kwa Joh Makini na
Dogo Janja na yote haya yataenda sambamba na bia zetu ambazo sasa tunauza
kwenye chupa mpya za ujazo 375ml kwa tsh 2000 tu,”
Naye Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya
Kaskazini, George Lugata alisema wao kama wadhamini wa mbio za kilometa 21
wamejiandaa vizuri kabisa. “Zoezila usajili limeenda vizuri na bila shaka mbio
hizi zimekuwa maarufu mno kwani watu wengi wamepata muamko wa kushiriki,”
alisema na kuongeza kuwa msisimko uliopo sasa hivi Moshi ndio huwafanya watu
wengi kuvutiwa.
Alisema watakuwa na promosheni
mbalimbali ndani ya uwanja ikiwa ni pamoja na kukutana na wateja wao kupitia
mbio za Kilimanjaro Marathon. “Tunaomba washiriki watembelee mabanda yetu
katika viwanja vya Chuo Cha Ushirika Moshi,” alisema.
Meneja Masoko wa GAPCO Caroline
Kakwezi alisema washiriki wao wote wa mbio za kilometa 10 kwa walemavu,
wanatarajiwa kuwasili kufikia Jumamosi jioni tayari kwa mashindano.
“Tumewalipia washiriki kutoka Dar es Salaam malazi, usafiri na chakula na wale
kutoka Arusha na Moshi tumewalipia usafiri ni matumaini yetu kuwa mbio za mwaka
huu zitakuwa na ushindani mkubwa kwani washiriki hawa wote walipatikana kwa
njia ya mchujo zoezi ambalo liliendesha na Kamati ya Paralimpiki Tanzania.
Meneja wa Grand Malt, Oscar
Shelukindo alisema kwa upande wa mbio za kilometa tano (fun run) maandalizi
yote yamekamilika na msisimko ni mkubwa. “Washiriki wetu watapata nafasi ya
kunywa Grand Malt ambacho ni kinywaji safi kwa afya,” alisema na kuongeza kuwa
wanatarajia washiriki wengikushinda mwaka jana.
Wadhamini wengine ni KK Security, TPC Limited, FNB,
Kibo Palace, Kilimanjaro Water, CMC Automobile, Rwandair, Keys Hotel and new
sponsors Anglo Gold Ashanti na KNAUF Gypsum.
Mbio za mwaka huu zinatarajiwa kufanyika katika
Viwanja vya chuo cha Ushirika Moshi (MuCO) kuanzia saa kumi na mbili asubuhi.
No comments