Yanga yaigagadua Comoro 5-1
Yanga |
Mwandishi Wetu, Comoro
WAWAKILISHI wa Tanzania katika mashindano ya Klabu Bingwa Afrika, Yanga, imeanza kwa vizuri safari yake ya kuwania ubingwa Afrika kwa kuichapa Ngaya Club de Mde kwa mabao 5-1 katika mchezo uliopigwa leo nchini hapa.
Ushindi huo, umeiweka sehemu nzuri Yanga kusonga mbele kabla ya mechi ya marudiano itakayopigwa Februari 18, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Yanga kama wakisonga mbele watakutana na mshindi kati ya Zanaco ya Zambia na APR ya Rwanda.
Mzambia Justin Zullu, Simon Msuva, Obren Chirwa, Amisi Tambwe na Thaban Kamusoko, ndiyo waliyowapa furaha mashabiki wa Yanga. Bao la wenyeji liliwekwa kimiani na Said Khalfan.
Katika mchezo huo ambao ulihudhuriwa na mashabiki wengi, timu hizo zilishambuliana kwa zamu na kuwafanya makipa wa pande zote mbili kuwa katika wakati mgumu.
Yanga ilifanya shambulizi lake la nguvu na kujiaptia bao dakika ya 43, baada ya Haji Mwinyi kutoa pasi ndefu iliyomkuta Chirwa ambaye alimsogezea pande safi Zullu aliyeusindikiza mpira wavuni.

Bao la pili kwa Yanga lilifungwa na Msuva baada ya kuonana vizuri na Haruna Niyonzima.
Dakika ya 59, Kamusoko alimchambua kipa wa Ngaya, Said Komandoo na kutoa pasi kwa Chirwa aliyeupeleka mpira wavuni.
Tambwe aliiongezea Yanga bao la nne dakika 65, akitumia vizuri pasi kutoka kwa Juma Abdul, kabla ya Ngaya kujipatia bao lake dakika ya 66, lililofungwa na Khalfan.

Dakika ya 73, Kamusoko alipata nafasi nzuri na kuifungia timu yake bao la tano kwa shuti kali la mbali, baada ya kupokea pasi nzuri kutoka kwa Niyonzima.
No comments