FAO YATOA SH. MILIONI 280 KATIKA MCHAKATO WA KUPITIA UPYA SERA YA TAIFA YA MISITU YA MWAKA 1998
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili
na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi ( kushoto) akizungumza kabla
kutia saini hati ya makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Shirika
la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) ya kupitia upya Sera
ya Taifa ya Misitu ya mwaka 1998 ambayo imekuwa ikitumika kwa
takribani miaka 19 hadi hivi sasa.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili
na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi ( kushoto) akiwa na Mwakilishi
wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) , Fred
Kafeero (kulia) wakisaini hati ya makubaliano ya kupitia upya Sera
ya Taifa ya Misitu ya mwaka 1998 ambayo imekuwa ikitumika kwa takribani
miaka 19 hadi hivi sasa.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili
na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi ( kushoto) akiwa na Mwakilishi
Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), Fred Kafeero
(kulia) wakibadilishana hati ya makubaliano ya kupitia upya Sera ya
Taifa ya Misitu ya mwaka 1998 ambayo imekuwa ikitumika kwa takribani
miaka 19 hadi hivi sasa.
Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na
Nyuki, Dkt. Ezekiel Mwakalukwa akionesha kitabu cha Sera ya Taifa ya
Misitu ya Mwaka ya 1998 ambayo imepitwa na wakati kutokana na
mabadailiko mengi kutokea nchini. Wengine ni Katibu Mkuu wa Wizara ya
Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi ( kushoto) akiwa na
Mwakilishi Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), Fred
Kafeero (kulia).
………………………………….
Serikali ya Tanzania na Shirika
la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) wameisaini makubaliano
ya kupitia upya Sera ya Taifa ya Misitu ya mwaka 1998 ambayo imekuwa
ikitumika kwa takribani miaka 19 hadi hivi sasa.
Akizungumza mara baada ya kusaini
makubaliano hayo leo jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Wizara ya
Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi amesema mpango huo
utagharimu kiasi cha shilingi milioni 280 ambazo zimetolewa na FAO kwa
ajili ya kufanya utafiti wa kuongezea takwimu ambazo zitaboresha Sera ya
Misitu ya Taifa ili iweze kufikia hadhi ya kimataifa.
Amesema hatua hiyo imekuja
Kutokana na Sera ya Misitu ya Taifa ya mwaka 1998 inayotumika hadi
hivi sasa kupitwa na wakati yakiwemo mabadiliko ya Kiuchumi,
Kuongezeka kwa idadi ya watu pamoja na Mabadiliko ya tabia ya nchi.
Maj. Gen. Gaudence ameeleza kuwa
kumekuwa na ongezeko kubwa la ufyekaji misitu na hivyo kumechangia
kupunguza uoto wa asili kutoka hekta milioni 55.9 kwa mwaka 1990 hadi
kufikia hekta milioni 46 kwa sasa lakini Sera ya Misitu ni ile ile.
‘’ Sera ya Taifa ya Misitu
ilishafanyiwa mapitio kuanzia mwaka 2009, Lakini kutokana na Sera hii
kukaa kwa muda wa takribani Miaka 9 hadi hivi sasa tumegundua kuwa
baadhi ya wadau wengi hawakupata nafasi ya kutoa mawazo yao. Hata wale
waliotoa mawazo yao mengi yameshapitwa na wakati.’’ Alisema Maj. Gen.
Milanzi
Naye Mwakilishi Shirika la
Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) , Fred Kafeero amesema kuwa
Mradi huo utasaidia wananchi wengi kushiriki na kutoa mawazo mengi
kuhusiana na Sera ya Misitu ikiwa pamoja na kuwajengea uwezo watumishi
kuweza kukusanya taarifa nyingi ili ziwezeshe kuboresha sera kupitia
tafiti.
Aidha,Kafeero amesema kutokana na
mabadiliko hayo FAO itasaidia katika kuhuisha sera mpya ambayo itatoa
majibu kwa changamoto zinazoikabili nchi hivi sasa na kukidhi mikataba
ya kimaifa kama vile mabadiliko ya tabia ya nchi
No comments