Header Ads

ad

Breaking News

DKT. KIGWANGALLA ATEMBELEA VITUO VYA TIBA YA DAWA ZA KULEVYA

indexNaibu wa Waziri wa Afya Dkt. Kigwangalla afanya ziara ya kushtukiza kwenye kituo cha kuwahudumia watu wanaotibiwa kuacha dawa za kulevya kwa kutumia methadone kilichopo Hospitali ya Mwananyamala ili kuona namna huduma zinavyotikewa. 
Ameamua kufanya ziara hiyo sababu kuna ongezeko kubwa la wateja siku za hivi karibuni kutokana na kuongezeka udhibiti. Na kuna taarifa kwamba wanaouza dawa za kulevya (drug dealers) wameathiriwa sana kwa kupoteza mapato ya sh bilioni 70 kwa uwepo wa vituo hivi ambavyo kwa sasa vinahudumia wateja 3351, na hivyo wameanza kubuni mbinu za kuwarudisha kwenye matumizi ya dawa za kulevya kwa mbinu mbalimbali ikiwemo kudai kuwa methadone haifanyi kazi.
Dkt. Kigwangalla ameagiza:
1. Hospitali zote za kanda zianzishe vituo vya rehab ndani ya miezi 6
2. Hospitali zote za mikoa nchini zianzishe kliniki ya kutoa methadone ndani ya miezi 6
3. Katibu Mkuu afya ahakikishe kuna Daktari bingwa wa afya ya akili kwenye kila mkoa ili kuanzisha na kusimamia vituo vya kutoa tiba ya methadone
4. Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kinondoni aongeze eneo la kliniki sambamba na watumishi kwenye kituo hiki 
5. Kamishna wa polisi wa operesheni maalum afuatilie wateja (exit follow-up) wanaotoka kliniki ili kudhibiti mkakati wa drug dealers wanaolenga kuwarubuni na kuwarudisha kwenye dawa za kulevya wateja wa vituo hivi. 
Msafara wa Dkt. Kigwangalla umeelekea Temeke Hospitali kwenye kituo kingine kama hiki.

No comments