CCM Z’BAR YATAKA SEKTA YA MICHEZO ISIINGIZWE ITIKADI ZA KISIASA
KATIBU wa Kamati Maalum wa Idara
ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar, Waride Bakar Jabu (kulia) akipokea
kwa niana ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai Kombe la
ubingwa la kutoka kwa Nahodha wa Timu hiyo , Suleiman Haroub
Suleiman“Bhaape” waliloshinda hivi karibuni dhidi ya Wasanii wa Zenj
fleva.
KATIBU wa Kamati Maalum wa Idara
ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar, Waride Bakar Jabu (kulia)
akikabidhiwa Mpira wa miguu kutoka kwa Nahodha wa Timu ya Tawi la CCM
Afisi kuu Zanzibar , Sualeiman Haroub Suleiman“Bhaape” katika hafla
iliyofanyika leo kufuatia ushindi wa hivi karibuni dhidi ya Timu ya
Wasanii wa Zenj fleva.
KATIBU wa Kamati Maalum wa Idara
ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar, Waride Bakar Jabu akikabidhiwa Jezi
kutoka kwa Nahodha wa Timu ya Tawi la CCM Afisi kuu Zanzibar ,
Sualeiman Haroub Suleiman“Bhaape” katika hafla iliyofanyika leo kufuatia
ushindi wa hivi karibuni dhidi ya Timu ya Wasanii wa Zenj fleva.
KATIBU wa Kamati Maalum wa Idara
ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar, Waride Bakar Jabu akiwahutubia
wafuasi wa CCM na Maafisa mbali mbali wa chama na jumuiya pamoja na
wachezaji wa timu ya Tawi la CCM Afisi Kuu Kisiwandui katika hafla
fupi ya kukabidhi kombe la ushindi kwa uongozi wa chama hicho.
Baadhi ya Maafisa wa CCM pamoja na
Katibu wa NEC Idara ya Itikadi na Uenezi Waride Bakari Jabu wakifurahia
ushindi wa Kombe hilo.
……………..
Na Is-haka Omar , Zanzibar.
ZIKIWA zimetimia siku 10 tangu
kuadhimishwa kilele cha kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi(CCM), ambapo
leo Timu ya Tawi la Chama hicho Kisiwandui imekabidhi rasmi Kombe la
ushindi kwa Katibu wa Kamati Maalum ya NEC, Idara ya Itikadi na Uenezi
Zanzibar, Waride Bakar Jabu.
Hafla hiyo imefanyika kufuatia
ushindi wa Timu hiyo kwa njia ya penaliti 4-2 dhidi ya timu ya Wasanii
wa muziki wa kizazi kipya Zenj Fleva katika mechi ya shamrashara za
kuadhimisha kuzaliwa kwa chama hicho.
Akizungumza katika hafla hiyo
Katibu wa Kamati Maalum ya NEC, Idara ya Itikadi na Uenezi Zanzibar,
Waride Bakar Jabu, amesema licha ya CCM kufanya shughuli za Kisiasa bado
inathamini mchango wa sekta ya michezo katika kuharakisha maendeleo ya
nchi.
Alisema harakati za Mapinduzi
Matukufu ya Zanzibar ya mwaka 1964 zilifanywa na vijana ambao wengi wao
walikuwa ni wanamichezo mashuhuri katika vilabu vya timu za hapa nchini.
Waride alieleza kuwa ushindi
waliotwaa timu ya Chama hicho ni miongoni mwa utekelezaji wa matakwa ya
Katiba ya CCM ibara ya 5 inayosisitiza ushindi kwa kila shughuli
inayofanywa chama hicho.
“Nakupongezeni sana timu yetu kwa
ushindi mliotwaa licha ya maandalizi ya mechi hiyo kuwa ya muda mfupi,
lakini kwa umoja na mshikamano wenu mmeweza kukijengea heshima kubwa
Chama katika sekta ya Michezo.
Nakuahidini kuwa Chama chetu
kitaendelea kuunga mkono juhudi zenu ili kuhakikisha taasisi yetu
inakuwa na timu ya mpira wa miguu yenye uwezo na nauomba uongozi wa timu
utafute mbinu ya kuanzisha timu za michezo mingine kwa lengo la kuweka
uwiano wa michezo kwa makundi yote”, .alieleza Waride.
Aidha alisema kwa niaba ya Niaba
ya Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai anatoa wito kwa vijana
kujiunga na michezo mbali mbali nchini kwa lengo la kuendeleza heshima
ya Zanzibar kimichezo.
Alisema Ilani ya Uchaguzi ya CCM
ya mwaka 2015/2020 inatambua umuhimu wa michezo katika kukuza na kuinua
uchumi na maendeleo ya nchi, hivyo ni miongoni mwa sekta inayotakiwa
kusimamiwa kikamilifu bila ya kuingiza mitizamo na itikadi za kisiasa.
Amezitaka taasisi zenye dhamana ya
Michezo nchini kujitathimini na kufanya utafti wa kuibua vikwazo
vinavyopelekea kukwamisha juhudi za maendeleo ya sekta hiyo na kutafuta
ufumbuzi wa kudumu kwa maslahi ya wananchi wote.
Mapema akisoma risala Afisa
mwandamizi wa Masuala ya Michezo na Ufundi wa Timu hiyo, Mzee Abdallah
Khatib ameupongeza uongozi wa Afisi kuu wa kuwaunga mkono toka mwanzo
walipowasilisha wazo la kuundwa kwa timu itakayocheza mechi ya
shamrashara ya kuzaliwa kwa CCM.
Alieleza kuwa pamoja na juhudi na
umoja ulipo ndani ya timu hiyo bado wanakabiliwa na changamoto ya
ukosefu wa vifaa vya michezo zikiwemo mipira, jezi, koni, dawa za
matibabu (first Aids Kit) na usafiri wa kuwafikisha katika sehemu
watakazokuwa wanaenda kucheza mechi za kirafiki.
Naye Meneja wa Timu hiyo Nadra
Juma Mohamed alisema lengo la kuanzisha timu hiyo ni kuendeleza umoja na
ushirikiano baina ya ngazi mbali mbali za Chama na Jumuiya ili kupata
sehemu mbadala ya kubadilishana mawazo.
“ Tunaomba ushirikiano kutoka kwa
viongozi wetu mbali mbali wakiwemo Wabunge, Wawakilishi na Madiwani waje
kutuunga mkono kwani jahazi tunalosafiria ni moja katika kulinda
maslahi ya chama chetu, huku tukiwa karibu na kundi la vijana
kimichezo.”, alisisitiza Meneja huyo.
Hata hivyo aliwashukru viongozi wa CCM na taasisi mbali mbali zilizosaidia kufanikisha mechi hiyo.
Akitoa Nasaha zake Kocha wa Timu
hiyo, Othman Kibwana aliuomba uongozi wa CCM Afisi kuu Zanzibar
kuwakutanisha na Timu mbali mbali zikiwemo za Bunge la Jamhuri ya
muungano, Baraza la Wawakilishi Zanzibar ili waweze kucheza nao mechi za
kirafiki kwa lengo la kudumisha mahusiano mengi kwa taasisi hizo.
Mechi hiyo iliyochezwa Februari 3
mwaka huu baina ya Timu ya Tawi la CCM Zanzibar na Wasanii wa Zenj
Fleva ambapo timu ya Chama hicho ilitwaa Kombe, pea moja ya jezi na
mpira mmoja wa miguu huku wapinzani wao wakipata pea moja ya jezi.
Hafla hiyo iliudhuriwa na Viongozi
mbali mbali wa Chama na Jumuiya akiwemo Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini
Kichama Bora afya Silima Juma, Katibu wa CCM Wilaya ya Mjini Fatma Juma
Shomari, Katibu Msaidizi Jumuiya ya Wazazi Zanzibar Mustafa Rashid
Malwa, Kaimu Afisa Utawala Mkuu wa CCM Zanzibar Mwenemzi Omar Said na
Katibu wa Idara ya Organazesheni CCM Zanzibar Haji Mkema Haji.
No comments