BENKI YA STANDARD CHARTERED YAKABIDHI VIFAA VYA MICHEZO KWA COCA COLA, MWANANCHI
Mkuu
wa Wateja Binafsi wa Benki ya Standard Chartered, Michael Shio (wa
kwanza kulia) akimkabidhi Mhariri Mtendaji wa Mwananchi Communication
Limited, Bakari Machumu (wa kwanza kushoto) vifaa vya michezo kwa ajili
ya mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017 (Road to Anfield)
ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 100 tangu benki hiyo kuanzishwa
mwaka 1917 yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Jumamosi hii jijini Dar
es Salaam. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa
Benki ya Standard Chartered, Juanita Mramba (wa pili kushoto) na Nahodha
wa timu ya Mwananchi Communication Limited ambaye ni bingwa mtetezi
Majuto Omary (wa pili kulia).
Mkuu
wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered, Juanita Mramba
(wa pili kushoto) akimkabidhi Mhariri Mtendaji wa Mwananchi
Communication Limited, Bakari Machumu (wa kwanza kushoto) vifaa vya
michezo kwa ajili ya mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017
(Road to Anfield) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 100 tangu
benki hiyo kuanzishwa mwaka 1917 yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi
Jumamosi hii jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia tukio hilo Mkuu wa
Wateja Binafsi wa Benki ya Standard Chartered, Michael Shio (wa kwanza
kulia) pamoja na kwa Nahodha wa timu ya Mwananchi Communication Limited,
Majuto Omar (wa pili kulia) wakati wa halfa fupi ya makabidhiano hayo
jijini Dar es Salaam.
Mkuu
wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered, Juanita Mramba
(wa kwanza kushoto) akimkabidhi Nahodha wa timu ya Mwananchi
Communication Limited, Majuto Omar ( kulia) seti ya jezi kwenye hafla
fupi ya makabidhiano iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia
tukio hilo ni Mkuu wa Wateja Binafsi wa Benki ya Standard Chartered,
Michael Shio (katikati).
Mkuu
wa Wateja Binafsi wa Benki ya Standard Chartered, Michael Shio (wa pili
kulia) akimkabidhi vifaa vya michezo Mwenyekiti wa timu ya Coca cola,
Samuel Mwakatumbula wa pili kutoka (wa pili kushoto) kwa ajili ya
mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017 (Road to Anfield) ikiwa
ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 100 tangu benki hiyo kuanzishwa mwaka
1917 yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi jumamosi hii jijini Dar es
Salaam. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki
ya Standard Chartered, Juanita Mramba (wa kwanza kushoto), Simon
Masanja mchezaji wa timu ya Coca cola (wa kwanza kulia) na Salehe Omar
mchezaji wa timu ya Coca cola (katikati).
Mkuu
wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered, Juanita Mramba
(kushoto) akimkabidhi mmoja wa wachezaji wa timu ya Coca cola, Simon
Masanja (kulia) vifaa hivyo vya michezo kwa ajili ya mashindano ya Kombe
la Standard Chartered 2017 (Road to Anfield) ikiwa ni sehemu ya
maadhimisho ya miaka 100 tangu benki hiyo kuanzishwa mwaka 1917
yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi jumamosi hii jijini Dar es Salaam.
Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mkuu wa Wateja Binafsi wa Benki ya Standard
Chartered, Michael Shio (wa pili kulia), Mwenyekiti wa timu ya Coca
cola, Samuel Mwakatumbula wa pili kutoka (wa pili kushoto) na Salehe
Omar mchezaji wa timu ya Coca cola (katikati).
Na Mwandishi wetu,
Benki
kongwe nchini Standard Chartered imekabidhi vifaa kwa timu za Mwananchi
Communication Limited na Coca cola kwa ajili ya mashindano ya ya Kombe
la Standard Chartered 2017 (Road to Anified) yaliyopangwa kufanyika
Jumamosi, kwenye viwanja vya JMK Park Kidongo Chekundu.
Mbali
ya kutafuta washindi wa kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya
Afrika Mashariki, mashindano hayo pia ni sehemu ya maadhimisho ya miaka
100 tangu benki hiyo kuanzishwa mwaka 1917.
Akizungumza
na waandishi wa habari wakati wa makabidhiano ya vifaa hivyo vya
michezo jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya
Standard Chartered, Juanita Mramba amesema jumla ya timu 32 kutoka
mashirika mbalimbali yanatashiriki katika mashindano hayo.
“Tunatarajia
timu 32 kushiriki hapa nchini na mshindi ataweza kuingia kwenye fainali
ya Kanda ya Afrika Mashariki itakayoshirikisha timu moja moja kutoka
Keny na Uganda, ambapo mshindi, atakwenda Liverpool kuangalia moja ya
mechi za ligi kuu ya Uingereza ya Liverpool na vile vile kushindana
katika mashindano mengine yatakayoshirikisha timu kutoka mabara ,”
alisema Mramba.
Mbali ya mashindano, mshindi pia atapata mafunzo ya siku tatu kujifunza mambo ya soka na kutoka kwa magwiji wa mashindano hayo.
Mramba
amesema kwamba benki hiyo ya Standard Chartered ilianzishwa mwaka 1917
na mwaka huu inatimiza miaka 100 tangu kuanzishwa kwake na imetenga
zaidi ya shilingi za kitanzania milioni 100 kwa ajili ya kusherehekea
siku yake ya kutimiza umri huo kwenye sekta ya kifedha.
Wakati
huo huo mmoja wa wachezaji waliowika miaka ya themanini na tisini wa
timu ya Liverpool, John Barnes atawasili nchini mwanzoni mwa mwezi Machi
tayari kwa mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017
yatakayohusisha timu za makampuni katika eneo hili la Afrika Mashariki.
Uzinduzi
wa awamu ya pili ya mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017,
yenye kauli mbiu “barabara ya kuelekea Anfield” inatarajiwa kutimua
vumbi kwenye viwanja vya Jakaya Kikwete Youth Park jijini Dar es
Salaam.
Katika uzinduzi huo timu mbili za wachezaji watano watano zitacheza kwa dakika kumi na mshindi atapewa zawadi.
Mashindano hayo ya Standard Chartered yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi Jumamosi hii kwenye viwanja vya JK Youth Park.
Yakiwa
katika mwaka wake wa sita, mashindano ya Kombe la Sndard Chartered
yamekuwa yakiimarika mwaka hata mwaka na kutoa washindi kutoka pande
zote za dunia. Mataifa ambayo yamenyakua kombe hilo ni pamoja na Kenya
(2016), Korea Kusini (2015) Vietnam (2014), Thailand (2013) na Singapore
(2012).
No comments