BARAZA LA VIONGOZI WA DINI LAUNGA MKONO JITIHADA ZA MAKONDA
Mwenyekiti wa Baraza la Viongozi wa Dini la Kupambana na Dawa za Kulevya Tanzania, Sheikh Alhad Mussa Salum.
Mwenyekiti
wa Baraza la Viongozi wa Dini la Kupambana na Dawa za Kulevya Tanzania,
Sheikh Alhad Mussa Salum (kushoto), akizungumza katika mkutano na
waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu baraza hilo kuunga mkono
jitihada za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda za kupambana na
wanaojihusisha na dawa za kulevya. Kulia ni Katibu wa Baraza hilo,
Padre John Solomon.
Baadhi ya viongozi wa dini (waliokaa), wakiwa kwenye mkutano huo. Wengine ni wanahabari.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.
Na Dotto Mwaibale
BARAZA la
Viongozi wa dini la kupambana na dawa za kulevya Tanzania ambalo liko
chini ya Tume ya kupambana na dawa za kulevya limeunga mkono jitihada
zinazofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda za kupambana
na watu mbalimbali wanaotumia dawa za kulevya.
Katika
hatua nyingine baraza hilo limeiomba serikali kumuongezea ulinzi
Makonda kwa kuthubutu kutaja watu wanaojihusisha kwa namna moja au
nyingine na dawa hizo.
Akizungumza
na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam leo, Mwenyekiti wa
Baraza hilo, Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Mussa Salum
,alisema Makonda anapaswa kuongezewa ulinzi kutokana na ujasiri
aliouonesha wa kuthubutu kuwataja kwa majina watu hao.
“Sisi
kama baraza tunapinga vita na kulaani hatua yoyote ya kushiriki katika
biashra au utimiaji wa dawa za kulevya kwa kuwa matumizi ya dawa hizo
yamekuwa ni kikwazo kikubwa cha maendeleo katika nchi yetu na
yanapotokea nguvu kazi ya Taifa kwa vile wahanga wakubwa wa matumizi ya
dawa hizi ni vijana”alisema.
Alisema
kutokana na ugumu wa kazi hiyo aliyoianzisha baraza hilo linamuombea kwa
mwenyezi mungu ili ampe ulinzi wake na kinga yake na azidi kumpa moyo
wa ujasiri wa kupambana na maovu yote yanayo haribu sifa ya Taifa letu
na vijana kwa ujumla.
Salum
alisema hivi sasa Makonda ameshanza kutengenezewa majungu, fitina na
uzushi mbalimbali ili kumkatisha tamaa na aonekane mbaya kwa watanzania
lakini hawatafanikiwa endapo atamtanguliza mwenyezi mungu katika
mapambano hayo.
Alisema
inawezekana wanaopinga au kubeza juhudi hizo ni kwa sababu tu madhara ya
dawa za kulevya hayajawagusa wao na familia zao hivyo hawana uchungu na
watanzania wenzao walioathirika hivyo wapuuzwe badala yake wasimame
pamoja kama watanzania dhidi ya vita hiyo.
Mwenyekiti
huyo wa baraza hilo alitumia fursa hiyo kuwaomba viongozi wengine waige
mfano wa Makonda wa kupambana na uovu huo mkubwa ambao ni janga kwa
Taifa kwani Tanzania bila dawa za kulevya inawezekana.
No comments