AWAMU YA PILI YA MAFUNZO YA WAJASILIAMALI WANAWAKE WA MKOA WA DAR ES SALAAM YALIO CHINI YA TAASISI YA MANJANO YAENDELEA
Mkufunzi
wa Maswala ya Biashara Ndugu Felix Maganjila Akitoa Mada kwenye Mradi
wa kuwejengea Uwezo wanawake Kwenye Ujasiriamali kupitia Taasisi ya
Manjano Foundation. Mafunzo hayo yalianza wiki iliyopita kwa lengo la
kuwajengea Uwezo wanwake wa Kitanzania kupitia bidhaa za vipodozi vya
LuvTouch Manjano. Washiriki wataweza kujisimamia na kujikita vizuri
kwenye biashara ya vipodozi na kujua mbinu mbalimbali za biashara kwa
lengo la kumjengea uwezo mwanamke wa Kitanzania.
Washiriki
wa Mafunzo ya Usajiriliamali na Urembo yalio chini ya Manjano
Foundation wakisiliza kwa makini mada mbalimbali kuhusu mafunzo hayo ya
kuwapa uwezo wa kuthubutu kufanya biashara, kujisimamia na kujua mbinu
mbalimbali za biashara.
Mkurugenzi
wa Taasisi ya Manjano Foundation, Shekha Nasser akiwa Katika Picha
ya Pamoja na Baadhi ya Washiriki walionufaika na Mradi huo.
Taasisi
ya Manjano Foundation, ambayo imeanzisha jukwaa kwa ajili ya kuandaa
miradi na programu ambazo zitamuinua mwanamke wa Kitanzania kwa
kumwondolea umasikini wa kipato na ambayo itakuwa ni chachu ya kubadili
uwezo wake ikiwa pamoja na kuisaidia jamii yake iliyomzunguka. Taasisi
hii limekwishazindua mradi wenye kubeba bendera yake, Manjano
Dream-Makers, mradi unaokusudia kuzaa kizazi kipya cha wajasiriamali
wanawake kwa kutumia kipodozi cha LuvTouch Manjano.
Awamu
ya Pili ya Mradi huu Ulizinduliwa na waziri wa Viwanda na Biashara Mh.
Charles Mwijage mnamo tarehe 14 Februari 2017, ambapo alisema
amefurahishwa sana wwa mwanamke wa Kitanzania kuzindua mradi
unaowawezesha wanawake kujiongezea kipato na kujiajiri hasa kwenye sekta
ndogo ya Urembo yenye fursa kubwa ya kukua.
No comments