Header Ads

ad

Breaking News

Yanga sasa yakaa sawa kileleni

Mshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa (kushoto) na Emmanuel Martin
Mwandishi Wetu

MSHAMBULIAJI wa kimataifa, Obren Chirwa kutoka nchini Zambia, ameiwezesha timu yake ya Yanga kushika usukani wa Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kuifungia mabao mawili dhidi ya Mwadui, mchezo uliopigwa Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Mabingwa hao watetezi wa ligi Bara, wamewapiga kumbo mahasimu wao, na kufanikiwa kufikisba pointi 46, huku wakiwaacha Simba na pointi zao 45. Simba jana ilichapwa bao 1-0 dhidi ya Azam FC.
Azam FC kwa ushindi huo iliendelea kubaki nafasi ya tatu na Kagera Sugar, nafasi ya nne zote zikiwa na pointi 34, zikitofautiana kwa uwingi wa mabao.
Chirwa ameibuka shujaa kwa kufunga mabao mawili na kufikisha mabao saba hadi sasa.

Katika mzunguko wa kwanza, Chirwa alibezwa na mashabiki wa timu hiyo, alifunga bao la kwanza dakika ya 70, ikiwa ni dakika sita tangu aingie kuchukua nafasi ya Haruna Niyonzima kwa kumalizia mpira uliotemwa na kipa, Shaban Kado kutokana na shuti kali la Simon Msuva.
Chirwa akiwa katika ubora, alifunga bao la pili dakika ya 85, akitumia vizuri mpira wa kichwa uliopigwa na Thaban Kamusoko.
 Kabla ya kufunga bao hilo, alimpiga chenga beki wa Mwadui ndani ya meta sita na kupiga shuti la mguu wa kushoto na kuwa bao la pili.
 Vikosi
Yanga: Deogratius Munishi, Juma Abdul, Hajji Mwinyi, Nadir Haroub, Kelvin Yondani, Zullu, Msuva, Kamusoko, Amis Tambwe/Said Juma dk 83, Niyonzima/Chirwa dk 64 na Kaseke/Emmanuel Martin dk 53.
 Mwadui: Kado, Nassor Masoud, Yassin Mustapha/David Luhenge dk 83, Malika Ndeule, Idd Mobby, Hassan Kabunda/Salum Kanoni dk 89, Razack Khalfan, Awadh Juma, Nonga, Salim Hamis/Joseph Kimwaga dk 86 na Seseme.
 Maechi nyingine za ligi hiyo, Mbao FC iliifunga Ruvu Shooting ya Pwani mabao 2-0 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, huku Majimaji ya Songea ikiizamisha Ndanda FC bao 1-0, kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea.

No comments