TRA YATWAA TUZO YA UBUNIFU WA MIRADI KWA SEKTA ZA AFRIKA
Meneja Mifumo ya Kielektroniki ya
Forodha kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Tinkasimile Felix
(kushoto) akipokea tuzo ya ubunifu wa mfumo wa TANCIS kutoka kwa Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Nchi na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi. Mindi Kasiga. Mfumo huu wa TANCIA
umeundwa kwa kuzingatia kanuni za hali ya juu za kiteknolojia kwa lengo
la kuongeza ufanisi, uharaka, uwazi na uhakika katika usimamizi wa
masuala ya forodha.
…………
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
imepata tuzo kutoka Umoja wa Afrika (AU) kutokana na mfumo wa Uondoaji
Mizigo Bandarini (TANCIS) ambao unafanya kazi kwa ufanisi na uharaka
zaidi pamoja na kudhibiti mia nyaya rushwa.
Tuzo hiyo imetolewa na Umoja wa
Nchi za Afrika jijini Addis Ababa Ethiopia, baada ya kufanyika
shindano la Taasisi za Serikali za Umoja wa Nchi hizo kutokana na
kuboresha mifumo ya utendaji kazi katika taasisi zao.
Akizungumza kwa niaba ya Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi. Mindi Kisiga
amesema kuwa TRA na Mamlaka ya Usimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya
Jamii(SSRA) ndiyo taasisi pekee za Serikali zilizoweza kufanya vizuri
katika ubunifu katika utendaji wa taasisi hizo.
“Tuzo hizi zinatolewa na nchi za
Umoja wa Afrika kwa taasisi za Serikali ambapo hushindanishwa katika
masuala ya ubunifu katika utendaji kazi wa taasisi husika,” alisema Bi.
Mindi.
Akizungumza kwa niaba ya Kamishna
Mkuu wa TRA Bw. Alphayo Kidata, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa
kodi toka Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Richard Kayombo alisema TRA
imeshinda tuzo hiyo kutokana na ubunifu wa mfumo wa TANCIS ambao
umeundwa kwa kuzingatia kanuni za hali ya juu za kiteknolojia kwa lengo
la kuongeza ufanisi, uharaka, uwazi na uhakika katika usimamizi wa
masuala ya forodha.
Alisema mfumo huu umeunganishwa na
mifumo mingine ya TRA ni ya wadau muhimu ambao wanahusika katika
uondoshaji wa bidhaa katika udhibiti wa forodha.
“Mfumowa TANCIS humwezesha
mwagizaji wa bidhaa kufuatilia hatua iliyofikiwa katika kuondosha bidhaa
zake kwa kutumia simu ya kiganjani au kifaa kingine chochote cha
kielektroniki hivyo mfumo huu unarahisisha utoaji huduma na kuongeza
ufanisi katika ukusanyaji wa mapato,” alisema Bw. Kayombo.
Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo
cha Mawasiliano toka Mamlaka ya Udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii
(SSRA) Bi. Sarah Kibonde alisema kuwa taasisi yake imepokea tuzo hiyo ya
ubunifu kwa kupitia mfumo wa kanzi data yaTaifa ya Sekta ya Hifadhi ya
Jamii.
Alisema TRA iliwawezesha kupata
taarifa zilizohusu walipaji kodi wa (PAYE) ambazo zilifanikisha
uchambuzi wa waajiri wasiochangia Mifuko yaJamii.
TRA na SSRA wameahidi kuendelea na
ubunifu zaidi ili kuhakikisha wanaendelea kubaki katika nafasi ya
ushindi na kufanya vizuri zaidi katika mashindano yajayo.
No comments