TAASISI YA MOYO YAPATA WAGENI KUTOKA VYUO VIKIKUU VYA WITWATERSRAND CHA NCHINI AFRIKA YA KUSINI NA MINESSOTA CHA NCHINI MAREKANI
Mkurugenzi
wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi na Prof.
Martin Valler Mkuu wa Kitivo cha Sayansi ya Afya wa Chuo kikuu cha
Witwatersrand cha Nchini Afrika ya Kusini wakiangalia jinsi upasuaji wa
bila kufungua kifua (Catheterization) unavyofanyika katika chumba Cath
Lab kilichopo katika Taasisi hiyo.
Mkurugenzi
wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akielezea
jinsi upasuaji wa Magonjwa ya Moyo unavyofanyika katika taasisi hiyo
wakati wageni kutoka Chuo kikuu cha Witwatersrand cha Nchini Afrika ya Kusini walipotembelea wodi aliyokuwa amelazwa mmoja wa wagonjwa aliyefanyiwa upasuaji. Kutoka kulia ni Prof.
Martin Valler, akifuatiwa na Afisa Muuguzi Roger Kibula, watatu kulia
ni Prof. Simon Nemutandani na wa pili kushoto ni Dkt. Marion Bergman.
Mkurugenzi
wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi
akiwaonyesha wageni kutoka Chuo kikuu cha Witwatersrand cha Nchini
Afrika ya Kusini sehemu
ya malipo ambapo wagonjwa wanalipia huduma. Wageni hao walitembelea
Taasisi hiyo hivi karibuni ili kuona huduma za matibabu ya moyo
wanazozifanya pia waliahidi kuimarisha mahusiano kati yao hii ikiwa ni pamoja na kutoa ufadhili wa masomo kwa madaktari wataokwenda kusoma katika chuo hicho.
Daktari bingwa wa Magonjwa ya Moyo na Mhadhili kutoka chuo Kikuu kishiriki cha Sayansi na
Tiba Muhimbili (MUHAS) Prof. Johnson Rwakatare akimuonyesha vipimo vya
moyo (ECHO) Prof. Martin Valler Mkuu wa Kitivo cha Sayansi ya Afya wa
Chuo kikuu cha Witwatersrand cha Nchini Afrika ya Kusini alipotembelea
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete hivi karibuni.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi
akiwaeleza wataalamu wa afya kutoka Chuo Kikuu cha Minnesota cha nchini
Marekani huduma za matibabu ya moyo wanazozitoa wakati walipoitembelea Taasisi hiyo hivi karibuni.
Picha na Anna Nkinda – JKCI
No comments