MAKAMU WA RAIS APOKEA TAARIFA YA TATHMINI YA UJENZI WA BOMBA JIPYA LA MAFUTA SAFI LA TAZAMA
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasikiliza Mawaziri wa
Nishati kutoka Tanzania na Zambia wakati wa kikao cha kupokea taarifa ya
tathmini ya ujenzi wa bomba jipya la mafuta safi kutoka Tanzania mpaka
Zambia, Mawaziri hao ni Waziri wa Nishati na Madini wa Tanzania
Mhe.Profesa Sospeter Muhongo (kulia) na Waziri wa Nishati wa Zambia Bw.
David Mabumba (kushoto), Ikulu jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya
pamoja na Waziri wa Nishati na Madini wa Tanzania Mhe.Profesa Sospeter
Muhongo (kulia) na Waziri wa Nishati wa Zambia Bw. David Mabumba
(kushoto) mara baada ya kumaliza mkutano wa kumpa taarifa Makamu wa Rais
ya tathmini ya ujenzi wa bomba jipya la mafuta safi, Ikulu jijini Dar
es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waziri wa
Nishati wa Zambia Bw. David Mabumba (kushoto) mara baada ya kupokea
taarifa ya tathmini ya ujenzi wa bomba jipya la mafuta safi
litakalotoka Dar es Salaam, Tanzania mpaka Ndola, Zambia, Ikulu jijini
Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya
pamoja na Ujumbe wa Tanzania na Zambia ambao ulifanya ziara ya kukagua
pampu na bomba la mafuta la TAZAMA kutoka Ndola, Zambia mpaka Dar es
Salaam Tanzania wakiongozwa na Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Profesa
Sospeter Muhongo na Waziri wa Nishati wa Zambia Bw. David Mabumba ambapo
walifanya tathmini ya ujenzi wa bomba jipya la mafuta safi litakalotoka
Dar es Salaam, Tanzania mpaka Ndola, Zambia.
No comments