WABUNGE WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI KUHAMASISHA JAMII JUU YA FURSA ZA KIBIASHARA ZINAZOPATIKANA AFRIKA MASHARIKI.
WABUNGE
wa Jumuiya la Afrika Mashariki kuanza kuhamasisha jamii ili kujua fursa
za Kibiashara zilizopo katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Ameyasema
hayo leo Mbunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Makongoro Nyerere
wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo,
amesema kuwa wataanza kuhamasisha jamii katika soko la Kariakoo na Soko
la Samaki la Feri jijini Dar es Salaam pamoja na vyombo vya habari
mbalimbali.
Makongo
amesema kusudi la kuelimisha jamii ili wafanyabishara waweze kufanya
biashara katika nchi za Afrika Mashari kama Kenya, Uganda, Rwanda na
Burundi.
Mbunge
wa Bunge la Afrika Mashari Makongoro Nyerere akizungumza na waandishi
wa habari(Hawapo pichani) jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na wabunge
wa bunge la Afrika Mashariki kuanza kuhamasisha jamii kuchangamkia fursa
za kibiashara zilizopo katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, Kutoka kulia
kwenda kushoto ni Mbunge wa bunge la Afrika Mashariki, Shyrose Banji,
Miriam Yahaya Usi, Ndarakilo Kessy na Dk.Twaha Tasilima wakiwa katika
mkutano huo leo.
Mbunge
wa Bunge la Afrika Mashariki, Abdullah Mwinyi (Katikati)akifafanua
jambo katika mkutano wa waandishi wa habari na wabunge wa bunge la
Afrika Mashariki leo jijini Dar es Salaam.
Mbune wa Bunge la Afrika Mashariki, Nderakilo Kessy (aliyesimama
)akizungumza na waandhishi wa habari hawapo pichani kuhusiana na wabunge
hao kuanza kuhamasisha jamii juu ya Fursa zilizopo katika jumuiya ya
Afrika Mashariki.
Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Shyrose Banji akizungumza kuhusiana na Fursa zilizopo katika Jumuiya ya Afrika Mashari.
Amesema kuwa frusa zilizopo kwa waalimu wa Lugha ya Kiswahili
wanaweza kwenda kufundisha Kiswahili kwenye Nchi za Afrika Mashariki
ikiwa ni Kenya Uganda, Rwanda, Burundi na Afrika ya kati ipo mbioni
kujiunga na Umoja huo.
Amesema Lugha ya Kiswahili kwa sasa imeanza kushika karibu nchi zote za Afrika Mashariki na hii ndio fursa Kubwa tuliyo nayo.
Picha na Avila Kakingo.
No comments