Header Ads

ad

Breaking News

TAKUKURU MKOANI PWANI YAZITAJA TAASISI NA IDARA 11 ZINAZOONGOZA KWA MALALAMIKO YA VITENDO VYA RUSHWA


Kamanda wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa Takukuru Mkoa wa Pwani Suzan Rymond akiwaonyesha waandishi wa habari ofisini kwake hawapo pichani orodha ya majina ya taasisi na idara ambazo zimeongoza kwa malalamiko ya vitendo vya rushwa (Picha na Victor Masangu)
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika mkutano huo wa Takukuru.

NA VICTOR MASANGU, PWANI

TAASISI ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU Mkoani Pwani imezitaja taasisi na idara zipatazo 11 ambazo zimelalamikiwa kuhusika katika matukio mbali mbali ya vitendo vya kupokea rushwa kinyume kabisa na sheria na taratibu za nchi.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake wakati akitoa taarifa ya utendaji kazi wa kipindi cha miezi mitatu kuanzia mwezi januari hadi machi mwaka huu Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Pwani Suzan Rymond alisema kuwa wale waliohusika watapeekwa katika vyombo vya sheria.

Susan alisema kwamba kwa sasa wamepokea jumla ya malalamiko 49 yanayohusina na vitendo vya rushwa baada ya kufanya uchunguzi waa wa wameweza kubaini idara inayoongoza kwa malalaamiko hayo kwa Mkoa mzima wa Pwani ni serikali za mitaa ambayo ina jumla ya malalamiko 18.

Kamanda huyo alifafafnua kuwa idara nyingine iliyoshika nafasi ya pili ilikuwa ni afya ambayo ilipata malalamiko 8,polisi 4,mahakama 3 ardhi 3 sekta binafsi 3 elimu 2 tanesco 2 fedha 1 vipimo 1 pamoja na maji 1.

“Ndugu zangu waandishi wa habari leo tumewaita ili kuwapa taarifa ua utekelezaji wa majukumu yetu kwa kipindi cha kuanzia mwezi januari hadi kufikia mwezi machi, na katika miezi hiyo tumepata malalamiko mengi yanayohusina na vitendo vya rushwa katika mkoa wetu wa Pwani.

Aidha Kamanda huyo alisema malalamiko ambayo wameshayapokea katika ofisi yaa ni 64 ambapo kati yao 49 ndio yanahusina na malalamiko ya vitendo vya upokeajiwa rushwa katika idara za serikali pamoja na taasisi mbali mbali.

Pia Suzan alisema kwamba kwa sasa katika kuhakikisha wanakomesha vitendo vya kupokea na kutoa rushwa wataendelea kufanya uchunguzi wa kina katika maeneo mbali mbali ili pindi watakapowabaini wahusika waweze kuwachukulia kali na kuwafikisha katika vyombo vya sheria.

Kamanda huyo alisema hadi sasa tayari kuna jumla ya kesi 22 zinazohusiana na vitendo vya rushwa ambazo zimeshafikishwa mahakamani,na pia bado kuna baadhi ya kesi nyingine bado zinafanyiwa uchunguzi zaidi.

Katika hatua nyingine Kamanda huyu aliwaomba wananchi wote wa Mkoa wa Pwani kuhakikisha wanatoa taarifa katika vyombo vinavyohusika endapo wakibaini kuna daily zoozte za mtu kutoa au kupokea rushwa ili sheria iweze kufuata mkondo wake wa kuwakamata wahusika ambao wamekuwa na tabia kama hiyo.

No comments