JUMLA YA DOLA MILIONI 20 ZA MAREKANI ZATUMIKA KUTENGEZA KIWANDA KIPYA CHA VINYWAJI VIKALI
Afisa
Habari wa kampuni ya nyati Spirit Tanzania,Alma Miraji akizungumza na
waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya vinywaji vya kiwanda cha
Nyati Spirit Tanzania havitakuwa madhara kwa mtumiaji kutokana na
kuthibishwa na shirika la viwango Tanzania (TBS) pamoja na mamlaka ya
chakula na dawa (TFDA) leo jijini Dar es Salaam kuliani Mkuu wa uhakiki
wa kiwanda hicho Karan Suchak.
Wafanyakazi
wa kiwanda cha Nyati Spirit Tanzania wakitoa maelekezo juu ya
kutotumia watoto walio chini ya umri wa miaka kumi na nane kutokana na
kuwa na kilevi kama ilivyo vinywaji vingine vikali .
Wafanyakazi wakiwanda hocho wakipanga vinywaji katika mabosi .(Picha na Emmanuel Massaka Globu ya Jamii)
Jumla
ya dola milioni 20 za Marekani zimetumika kwa ajili ya kutengeza kiwanda
kipya cha vinywaji vikali maarufu kama nyati spirit Tanzania .
Akizungumza
wakati wa uzinduzi huo mkuu wa uhakiki wa kiwanda hicho Karan Suchak
amesema kuwa pamoja na kuingia katika soko la ushindani la vinjwaji
vikali pia ni kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano ya
kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda ambapo watanzania zaidi ya mia
moja wamepata ajira huku idadi yao ikitarajiwa kuongezeka.
Kwa
upande wa afisa habari wa kampuni hiyo Alma Miraji amesema kuwa vinywaji
hivyo havitakuwa na madhara kwa mtumiaji kutokana na kuthibishwa na
shirika la viwango Tanzania (TBS) pamoja na mamlaka ya chakula na dawa
(TFDA) huku wakikusudia kuweka nembo maalumu itayotenganisha na bidhaa
nyingine feki.
Alma
ameongeza kuwa vinywaji ambavyo vinapatikana kwa ladha tofauti ikiwemo
kahawa matunda havitoruhusiwa kutumiwa na watoto walio chini ya umri wa
miaka 18 kutokana na kuwa na kilevi kama ilivyo vinywaji vingine.
No comments