WANAWAKE WAASWA KUJITOKEZA KWA WINGI KUKIPIGIA KURA CHAMA CHA MAPINDUZI
Wanawake
wameaswa kukipenda chama cha mapinduzi kwakuwa ndicho chama pekee
kitakachowaletea maendeleo yanayotakiwa kwakuwa kinajua changamoto
zinazo wakabili wananchi katika kipindi hiki.
Akizungunguza
na wanawake wa wa Kata ya Makolongoni Mbunge wa viti maalum mkoani
Iringa Rose Tweve aliwataka wananchi kutobabaishwa na wapinzani kwani
hawana nia njema na watanzania na kusema kuwa chama hicho kina misingi
ya kutetea amani ya Nchi.
"sisi
sote ni wanawake niwaombeni sana tukipigie kura chama cha mapinduzi
kiweze kupata ushindi wa kishindo leo katika chama kuna mgombea mwenza
mwanamke tazama hamsini kwa hamsini wahamasisheni vijana wenu pia
waelezeni mazuri yalimo ndani ya ccm bila kuwaambia wataendelea kurub
uniwa na kutumiwa kwa faida za wachache" alisema rose
Alisema
huu ndiyo wakati wa wanawake kujitokeza kwa wingi kukiunga mkono chama
cha mapinduzi kwa kuwapigia kura wagombea wanaotokana na chama hicho
kwakuwa kukipa nchi chama cha Upinzani ni kujisaliti wenyewe hiyo
aliwaomba wanawake kuhakikisha wanakisaidia chama cha mapinduzi kiweze
kushinda.
No comments