MGODI WA DHAHABU WA BULYANHULU, BGML, WAKABIDHI MIRADI YA THAMANI YA SHILINGI BILIONI MOJA WILAYA YA MSALALA
Kaimu
Mku wa Wilaya ya Msalala, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kahama mkoani
Shinyanga, Benson Mpesya, Meneja Mkuu Mgodi wa Dhahabu Bulyanhulu, BGML,
Michelle Ash, (katikati) na Mkurugenzi wa Maendeleo Halmashauri ya Wilaya ya
Msalala, wakipapu maji wakati wa uzinduzi rasmi wa kisima kirefu cha maji
kilichojengwa kwa ufadhili wa kampuni hiyo huko Bugarama. BGML, inayomilikiwa
na Kampuni ya Acacia, imekabidhi miradi mine ya elimu na maji kwa Halmashauri
hiyo yote ikiwa na thamani ya shilingi Bilioni 1.
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Msalala, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, Benson Mpesya, (kushoto), akiongozana na Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu ulioko wilaya ya Msalala Mkoani Shinyanga, Michelle Ash, (katikati), na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Busindi, Joseph Misungwi, baada ya kuzindua moja kati ya nyumba kadhaa za walimu, zilizojengwa kwa msaada wa mgodi huo. Mhgodi huo unaomilikiwa na kampuni ya uchimbaji na utafutaji madini, Acacia, umekabidhi halmashauri ya wilaya hiyo, miradi ya elimu na maji yenye thamani ya shilingi Bilioni 1, kwenye hafla hiyo iliyofanyika Agosti 31, 2015.
MOJA
kati ya majengo ya shule ya Msingi Busindi, yaliyomaliziwa kujengwa na
mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu ulioko wilaya ya Msalala mkoani
Shinyanga. Mgodi huo unaomilikiwa na kampuni ya Acacia, umekabidhi
miradi minne ya elimu na maji yenye thamani ya shilingi bilioni 1 ikiwa
ni sera ya kampuni kujenga mahusiano mema na jamii inayozunguka migodi.
NA
K-VIS MEDIA
MGODI
wa dhahabu wa Bulyanhulu, BGML, Jumatatu Agosti 31, 2015, umekabidhi miradi,
yenye thamani ya shilingi Bilioni Moja kwa Mamlaka ya Halmashauri ya Wilaya ya
Msalala mkoani Shinyanga.
Akizungumza
kwenye hafla ya kukabidhi miradi hiyo, Meneja Mkuu wa Mgodi huo unaomilikiwa na
Kampuni ya uchimbaji madini, Acacia, Michell Ash, alisema, “Sisi BGML tulitoa
ufadhili wa kugharimia miradi ya kijamii kwa wenyeji wetu na leo tunakabidhi
miradi hiyo minne baada ya kukamilika kwake ikiwa ni ishara ya muendelezo wa
utekelezaji wa ahadi zetu za kampuni kuwajibika kusaidia jamii.” Alisema.
“Ninayo
furaha kuu kutangaza kuwa BGML ilifadhili miradi minne kwa thamani ya shilingi
bilioni 1,100,546,766 na tunatarajia kutoa fedha zaidi mwaka huu kusaidia sekta
za Afya na Elimu.”Alifafanua.
No comments