DOUBLE TREE HOTEL WATOA MSAADA KWA KITUO CHA WATOTOT WETU TANZANIA
Meneja
Mkuu wa Double Tree hotel Ndugu Ian Mclachlan Akimkabidhi Mkuu wa
Wilaya ya Kinondoni Mh Paul Makonda Msaada wa Magoro 80 .Akipokea Msaada
huo Mkuu wa Wilaya Mh Makonda ameushukuru Uongozi wa Msaada huo.Kutoka
Hotel ya Double Tree ya Jijini Dar es salaam.Msaada huo umekabidhiwa na
Mkuuwa Wilaya ya Kinondoni Mh Paul Makonda.Kituo Hicho kinacholea Watoto
na vijana wa Mitaani na wanaoishi katika Mazingira Magumu kina Jumla ya
Watoto Pamoja na Vijana 120 Kilianzishwa Mnamo mwaka 1998 Kwa lengo la
Kuwasaidia watoto waliokosa Malezi na Huduma Mbalimbali za
Kijamii.Kituo Hicho kinapatikana Kimara Suka pamoja na Kijiji cha
Mazizini msata wilayani Bagamaoyo kinakabiliwa na Changamoto Mbalimbali
hivyo Uongozi wa Kituo Hicho kinawaomba Watu binafsi na Wafadhili
Mbalimbali kujitokeza kuwasaidia
Mkuu
wa Wilaya ya Kinondoni Mh Paul Makonda akimkabidhi Mkurugenzi wa Kituo
cha Watoto wetu tanzania Ndugu Evans Tegete Msaada uliotolewa na
Uongozi wa Double Tree Hotel .
Kituo
cha Watoto wetu Tanzania leo kimepokea Msaada wa Magodoro 80 .Mkuu wa
Wilaya Mh Makonda ametaka Uongozi wa Kituo cha Watoto Wetu tanzania
Msaada huo Kuwanufaisi watoto wa Kituo hicho na Kuutunzaili uweze
kusaidia watu wengi zaidi.
Mkuu
wa Wilaya ya Kinondoni Mh Paul Makonda Katika Picha na Meneja Mkuu wa
Double Tree hotel Ndugu Ian Mclachlan (kushoto) Pamoja na Mkurugenzi wa
Masoko na Mauzo wa Hotel ya Double tree Ndugu Florenso Kirambata
Mkurugenzi
wa Masoko na Mauzo wa Hotel ya Double tree Ndugu Florenso Kirambata
Akieleza jambo wakati Kukabidhi Msaada huo.Ikumbukwe Mkurugenzi wa
Masoko na Mauzo wa Hotel ya Double Ndiye aliyefanikisha Kupatikana kwa
Msaada huo Mara baada ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Paul Makonda
Alipotembelea Kituo cha Watoto wetu Tanzania na Kujionea Changamoto
zilizokuwa zinawakabili watoto hao hao ndipo alipoamua Kumshirikisha
Mkurugenzi huo ambaye Ameweza Kuushawishi uongozi wa Hoteli Hiyo kutoa
Msaada huo ikiwa ni sehemu Msaada kwajili ya Jamii inayoizunguka Hotel
hiyo. Mkurugenzi
wa Kituo cha Watoto wetu tanzania Ndugu Evans Tegete Akitoa Neno la
shukrani mara baada ya Kupokea Msaada huo ambapo aliushukuru Uongozi wa
Double tree hotel kwa Msaada huo Pamoja na Mkuu wa Wilaya aliyetembelea
Kituo hicho na Kujionea Changamoto zinazowakabili.
Mkuu
wa Wilaya ya Kinondoni Mh Paul Makonda Katika Picha na Meneja Mkuu wa
Double Tree hotel Ndugu Ian Mclachlan (kushoto) Pamoja na Mkurugenzi wa
Masoko na Mauzo wa Hotel ya Double tree Ndugu Florenso Kirambata
No comments