Header Ads

ad

Breaking News

Yanga yalewa Sukari Kagera




Na Timzoo Kalugira, Bukoba

MABADIRIKO ya Kocha Mkuu wa timu ya Kagera Sugar, Abdallah Kibadeni ya kumtoa Darlington Enyima na kumuingiza Temi Felex dakika ya 57, ndio yaliyowapa ushindi wa bao 1-0, Kagera Sugar, kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba. 
licha ya mchezo huo kuwa wa kushambuliana kwa zamu, lakini Yanga walijikuta wakifungwa bao hilo pekee dakika 67, kupitia kwa Felex kwa shuti kali lililomshinda kudaka kipa Yaw Berko.

Dakika ya tisa, Enyima, alikosa bao la wazi baada ya shuti kupanguliwa, na dakika ya 15, Amandusi Nesta aliokoa mpira uliokuwa ukielekea nyavuni uliopigwa na Haruna Niyonzima, huku kipa Andrew Mtala akiwa amepotea.
Baada ya  mchezo kumalizika, daktari wa timu ya Yanga,  Juma Sufian, aliwarushiakiti kwa hasira mashabiki wa waliokuwa jukwaani, wakati wakimlaumu mwamuzi.

Mbali na Sufiani, wachezaji wa Yanga, Didie Kavumbagu, nahodha wao,  Nadir Haroub 'Cannavar' na Jerryson Tegete, walipigana na mashabiki aliyekuwa amevaa fulana yenye rangi wanazotumia Manchester United ya England, wakati wakielekea kwenye vyumba vya kubadilishia nguo.

Yanga: Yaw Berko, Juma Abdul, Stephan Mwasyika, Nadir Haroub 'Cannavaro', Mbuyu Twite, Athuman Idd 'Chuji', Nizar Khalfan, Frank Domayo, Didier Kavumbagu, Said Bahanunzi/Jerrson Tegete na Haruna Niyonzima.

Kagera Sugar: Andrew Mtala, Juma Nande, Salum Kanoni, Amandusi Nesta, Benjamin Afee, Maregesi Mwangi, Daud Jumanne, George Kavila, Darling Enyima, Shija Mkina na wilifred Amer.

ciao

No comments