TFF yaipiga faini Yanga ya sh. milioni tatu
![]() |
Kikosi cha Yanga |
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF),
limeitahadharisha klabu ya Yanga kuvaa jezi zenye nembo ya mdhamini katika
mechi zake za Ligi Kuu Tanzania Bara, kwa mujibu wa mkataba kati ya TFF na
mdhamni mkuu wa ligi hiyo, kampuni ya simu ya Vodacom.
TFF, imefikia hatua hiyo ya
kuitaka Yanga kuvaa jezi hizo, baada ya mabingwa hao wa Afrika Mashariki na
Kati kucheza mechi mbili bila kuvaa jezi mpya zenye nembo za mdhamini huyo.
Akizungumza na waandishi wa habari
jijini Dar es Salaam leo, Katibu Mkuu
wa TFF, Angetile Osiah, alisema kutokana Yanga kukiuka masharti hayo, wameitozwa
faii ya sh. milioni 3, kwa mechi hizo mbili, ambapo adhabu hiyo inaweza
kuongezeka baada ya kikao cha Kamati ya Ligi kukaa.
“Tunatarajia kuwaandikia
Yanga barau ya kuwatoza faini ya sh. milioni 3, kwa kucheza mechi mbili bila ya
kuvaa jezi zenye nembo ya mdhamini,” alisema Osiah.
Licha ya mdhamini huyo kutoa
vifaa kwa timu zote za ligi kuu, Yanga walishindwa kuzitumia jezi hizo kwa kuwa
zina nembo ya mdhamini ina rangi nyekundu na nyeupe, ambazo zinatumiwa na mahasimu
wao, Simba.
Kutokana na hilo, Osiah
alisema Yanga walilazimika kuwasiliana na mdhamini ili awabadilishie nembo
hiyo, lakini juhudi hizo ziligonga mwamba.
“Kikubwa Yanga hawataki kuvaa
jezi zenye nembo nyeupe na nyekundu, kwa madai kuwa, hizo rangi zinazotumiwa na
mahasimu wao, lakini mdhamini hajakuliana nao, hivyo TFF tumelazimikia kuwasihi
wana Jangwani hao,” alisema Osiah.
Osiah alisema lengo la
kuwasihi Yanga kuvaa jezi hizo, ni kutaka kuinusuru timu hiyo na adhabu ya
kushushwa daraja, kwa mujibu wa kanuni za ligi.
“Moja ya adhabu ambayo Yanga itawakumba, ni kushushwa daraja kwa
mujibu wa kaninu za ligi, ndio maana tunalazimika kuwasihi kabla ya kukumbwa na
adhabu hiyo” alisema Osiah.
ciao
No comments