Simba, Oljoro JKT zaingiza sh. milioni 46/-
![]() |
Mnyama, Simba Sports Club |
Pambano la
Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Simba na Oljoro JKT ya Arusha lililochezwa jana
(Oktoba 7 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa wenyeji
kuibuka na ushindi wa mabao 4-1 limeingiza sh. 46,680,000.
Watazamaji
8,081 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo kwa viingilio vya sh. 5,000, sh.
8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh.
8,172,396.61 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh.
7,120,677.97.
Mgawo
mwingine wa mapato hayo ni posho ya msimamizi wa kituo sh. 120,000, kamishna wa
mechi sh. 193,000, waamuzi sh. 210,000, mwamuzi wa akiba (reserve referee) sh.
70,000, usafi na ulinzi wa uwanja sh. 2,350,000 na Wachina (stadium technical
support) sh. 2,000,000.
Umeme sh.
300,000, maandalizi ya uwanja (pitch preparation) sh. 400,000, ulinzi wa mechi
sh. 3,500,000 wakati tiketi ni sh. 3,175,000. Gharama za mchezo sh.
2,724,132.20, uwanja sh. 2,724,132.20, Kamati ya Ligi sh. 2,724,132.20, Mfuko wa
Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 1,634,479.32 na Chama cha Mpira wa Miguu
Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,089,652.88.
PONGEZI KWA
UONGOZI MPYA ARFA
Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linatoa pongezi kwa uongozi mpya wa Chama cha
Mpira wa Miguu Mkoa wa Arusha (KRFA) uliochaguliwa katika uchaguzi uliofanyika
jana (Oktoba 7 mwaka huu).
Ushindi
waliopata viongozi waliochaguliwa kuongoza chama hicho unaonesha jinsi wajumbe
wa Mkutano Mkuu wa ARFA walivyo na imani kubwa kwao katika kusimamia mchezo huo
mkoani Kigoma.
TFF inaahidi
kuendeleza ushirikiano wake kwa Kamati ya Utendaji ya ARFA chini ya uenyekiti wa
Khalifa Mgonja ambaye amechaguliwa tena kuongoza chama hicho.
Uongozi huo mpya una changamoto nyingi,
kubwa ikiwa ni kuhakikisha unaendesha shughuli za mpira wa miguu mkoani Arusha
kwa kuzingatia katiba ya ARFA pamoja na vyombo vya mpira wa miguu vilivyo juu
yake.
Pia tunatoa
pongezi kwa Kamati ya Uchaguzi ya ARFA na Kamati ya Uchaguzi ya TFF kwa
kuhakikisha uchaguzi huo unaendeshwa kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi za
wanachama wa TFF.
Viongozi waliochaguliwa katika uchaguzi huo
ni Khalifa Mgonja (Mwenyekiti), Seif Banka (Makamu Mwenyekiti), Adam Brown
(Katibu), Peter Temu (Mjumbe wa Mkutano Mkuu TFF), Omari Walii (Mwakilishi wa
Klabu TFF) na Mwalizo Nassoro (Mhazini).
Ofisa
Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
No comments