Sabi alilia kuchezewa ‘rafu’ uchaguzi UVCCM Mara
KAPSHENI: Aliyekuwa
mgombea nafasi ya Uenyekiti wa Umoja wa Vijana Mkoa wa Mara, Gabriel Mnasa Sabi
(kulia) akifafanua jambo wakati alipozungumza na waandishi wa habari kuhu
Na
Mwandishi wetu
ALIYEKUWA
mgombea nafasi ya Uenyekiti wa Umoja wa Vijana Mkoa wa Mara, Gabriel Mnasa Sabi
ameuomba uongozi wa juu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) pamoja na Umoja wa Vijana
makao makuu, kuingilia kati chaguzi za umoja ambazo zimetawaliwa na vitendo vya
hujuma na rushwa.
Sabi
ambaye juzi aishindwa kwa tofauti ya kura 14 dhidi ya Ditu Manko , alisema kuwa
uchaguzi wao haukuwa huru na haki kwani matokeo yalijulikana kabla ya kupiga
kura.
Alisema
kuwa alitangaziwa matokeo hayo wakati wa kampeni kwa madai kuwa nafasi ya
uenyekiti lazima itoke wilaya ya Tarime kutokana na nguvu ya kifedha.
“Hali
hiyo ilinifanya kunyong’onyea hata kabla ya uchaguzi, hata hivyo nilipiga moyo
konde na kuingia kwenye uchaguzi, matokeo yakawa yaleyale, nilishangazwa sana
na wafuasi wangu wakaamua kutoendelea na uchaguzi huo,” alisema Sabi.
Alisema
kuwa baada ya matokeo hayo, fujo zikaanza kwani wafuasi wake walichoka kuona
vitendo vya uonevu vya waziwazi na kuongeza kuwa pamoja na wafuasi wake kutoka,
uchaguzi huo uliendelea na kuhoji hao waliochaguliwa walipata kura hizo kwani
sidhani kama idadi ya wapiga kura kwa mujibu wa katiba ilifikiwa.
“Kasoro
hizi si za kuziacha kwani zinawagawa wanachama, ni lazima zikemewe kwani
bado kuna chaguzi nyingi ndani ya chama,” alisema.
Alifafanua
kwa kusema kuwa hana tatizo na uongozi wa juu wa CCM kutokana na sera madhubuti
zenye kuleta maendeleo ya nchi, ila kilio chake ni viongozi wanaokipaka matope
chama hasa wa ngazi ya chini.
No comments