Push Mobile yamzawadia mshindi wa Serengeti Fiesta 2012 magari mawili
Na
Mwandishi wetu
KAMPUNI
ya Push Mobile imemkabidhi Diana Elisa Mkoba Magari mawili aina ya
Vitz yenye thamani ya shs million 16 kufuatia promosheni iliyoendeshwa
wakati wa tamasha la Fiesta katika mikoa mbali mbali ya Tanzania Bara.
Magari
hayo yalikabidhiwa na Meneja Mauzo na Masoko wa Push Mobile, Rodney Rugambo
katika hafla fupi iliyofanyika jijini.
Rugambo
alisema kuwa wamefarijika kuwa wadhamini wasaidizi wa tamasha hilo lililodhaminiwa
na bia ya Serengeti kutokana na kutoa mchango wao katika jamii, hasa kwa
kupitia muziki wa kizazi kipya.
Alisema
kuwa zawadi hiyo ya magari mawili ni itimisho la magari sita waliyotoa katika
mikoa mbali mbali wakati wa tamasha hilo. Kampuni hiyo ilitoa gari moja moja
mikoa ya Kilimanjaro, Mbeya, Mwanza na Dodoma.
Mbali
ya zawadi hizo, kampuni hiyo pia ilitoa zawadi ya pikipiki 15, simu ya mkononi
aina ya Nokia dabodabo 130, simu aina ya blackbey 14 na washindi wa fedha
taslim shs milioni 20. Thamani ya vitu vyote hivyo ni milioni 200.
“Ni
matarajio yetu kuwa Diana atayatumia magari haya ipasavyo na tunampongeza kwa
ushindi, watu wengi walishiriki katika bahati nasibu hii na Diana kubahatika
kushinda magari mawili, tunawaomba wadau washiriki katika promosheni zetu
nyingine,” alisema Rodney.
Diana
alisema kuwa amefurahi kushinda zawadi hiyo kwani hakuamini baada ya kupokea
simu ya ushindi wa zawadi hizo. Alisema kuwa kwa vile yeye ni mwanafunzi
wa chuo cha Bandari atatumia gari moja na lingine atajua wapi kulipeleka, kama
Kagera kwa mama yake au libaki hapa hapa Dar es Salaam.
No comments