PONGEZI KWA UONGOZI MPYA ARFA
![]() |
Msemaji wa TFF, Boniface Wambura |
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linatoa pongezi kwa uongozi mpya wa Chama cha
Mpira wa Miguu Mkoa wa Pwani (COREFA) uliochaguliwa katika uchaguzi uliofanyika
jana (Oktoba 14 mwaka huu).
Ushindi
waliopata viongozi waliochaguliwa kuongoza chama hicho unaonesha jinsi wajumbe
wa Mkutano Mkuu wa COREFA walivyo na imani kubwa kwao katika kusimamia mchezo
huo mkoani Pwani.
TFF
inaahidi kuendeleza ushirikiano wake kwa Kamati ya Utendaji ya COREFA chini ya
uenyekiti wa Hassan Othman Hassan ambaye amechaguliwa tena kuongoza chama
hicho.
Uongozi
huo mpya una changamoto nyingi, kubwa ikiwa ni kuhakikisha unaendesha shughuli
za mpira wa miguu mkoani Pwani kwa kuzingatia katiba ya COREFA pamoja na vyombo
vya mpira wa miguu vilivyo juu yake.
Pia
tunatoa pongezi kwa Kamati ya Uchaguzi ya COREFA na Kamati ya Uchaguzi ya TFF
kwa kuhakikisha uchaguzi huo unaendeshwa kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi za
wanachama wa TFF.
Viongozi
waliochaguliwa katika uchaguzi huo ni Hassan Othman Hassan (Mwenyekiti), Riziki
Majala (Katibu), Geofrey Irick Nyange (Mjumbe wa Mkutano Mkuu TFF), Juma Haruna
Kisoma (Mwakilishi wa Klabu TFF) na Abubakar Allawi (Mhazini).
Waliochaguliwa
kuwa Wajumbe wa Kamati ya Utendaji katika uchaguzi huo uliofanyika kisiwani
Mafia ni Musa Bakari Athumani, Godfrey Magnus Haule na Gwamaka Oden
Mlagila. Mwakilishi wa Wanawake ni Florence Ambonisye.
No comments