MISRI NAYO YAIKACHA SERENGETI BOYS
Timu
ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) imefuzu
kucheza raundi ya tatu nay a mwisho kwenye michuano ya kutafuta tiketi ya
kucheza Fainali za Afrika kwa Vijana baada ya Misri kujitoa.
Serengeti
Boys ilikuwa icheze raundi ya pili dhidi ya Misri; mchezo wa kwanza ukichezwa
Oktoba 14 mwaka huu jijini Dar es Salaam na ule wa marudiano wiki mbili baadaye
jijini Cairo.
Katika
raundi ya kwanza Serengeti Boys inayofundishwa na Jakob Michelsen kutoka
Denmark ilikuwa icheze na Kenya mwezi uliopita, lakini nchi hiyo ilijitoa
katika michuano hiyo ambayo fainali zake zitachezwa Machi mwakani nchini
Morocco.
Serengeti
Boys sasa itacheza raundi ya tatu kwa kumkabili mshindi wa mechi kati ya
Zimbabwe na Congo Brazzaville. Mechi ya kwanza itachezwa Novemba 18 mwaka huu
jijini Dar es Salaam wakati ya marudiano itafanyika ugenini wiki mbili baadaye.
Zimbabwe
na Congo Brazzaville zitapambana zitapambana kati ya Oktoba 12-14 mwaka huu,
Zimbabwe ikiwa mwenyeji wa mechi ya kwanza wakati ya marudiano itafanyika kati
ya Oktoba 26-28 mwaka huu.
No comments