Makamu wa Rais wa FA Senegal, abwaga manyanga
![]() |
Louis Lamotte |
DAKAR, Senegal
MAKAMU wa Rais wa Shirikisho la Soka
la Senegal, Louis Lamotte, amejiuzulu wadhifa wake juzi, baada ya fujo
zilizozuka kwenye mechi mjini Dakar na kutolewa kwa nchi hiyo kwenye michuano
ya Mataifa ya Afrika mwaka 2013.
“Kama mwanachama wa kamati ya mechi
hiyo kati ya Senegal na Ivory Coast, siwezi kuendelea na majukumu kwa kile
kilichotokea uwanjani Jumamosi. Hivyo, nafikiri kitu cha kwanza cha kufanya ni
kujiuzulu,” alisema Lamotte, akiwaambia waandishi wa habari mjini Dakar.
“Pia, naondoka na kutoa nafasi kwa ajili
ya uchunguzi kutokana na fujo zilizotokea.”
Lakini, Rais wa shirikisho hilo, Augustin
Senghor, Jumatano iliyopita aliahidi kutojiuzulu kutokana na tukio hilo la
vurugu.
Tayari, Ivory Coast wametangazwa
rasmi kuwa, washindi wa mechi hiyo, ambayo ilimalizwa, kabla ya muda wake,
wakati wageni wakiwa mbele kwa mabao 2-0, yaliyofungwa na Didier Drogba.
No comments