Header Ads

ad

Breaking News

Lucy Miss awa Miss Photogenic, atinga 16 Bora Miss Tanzania


ucy Stephano

Na Mwandishi Wetu, Monduli

Redds MISS Mbulu, Lucy Stephanojuziusikualifanikiwakukatatiketiyakuingia 16 bora yaRedd’s Miss Tanzania, baada ya kufanikiwa kutwaa taji la ReddsMiss Photogenic.
 ShindanohilolilifanyikakatikaUkumbiwaEmanyata Lodge, uliopo mjini hapa.
 Lucy, alifanikiwa kuwashinda warembo wengine 30 wanaoshiriki ReddsMiss Tanzania na kufanikiwa kutwaa taji hilo.
 Mrembo huyo alifanikiwa kulitwaa taji hilo, baada ya ushindani mkali uliokuwepo kati yake na Redds Miss Dar Indian Ocean, Diana Hussein na ReddsMiss Ilala namba mbili, Magdalena Roy.
 Kutokana na kufanikiwa kwak ekutwaa taji hilo, Lucy amefanikiwa kuvuka hatua moja kubwa zaidi ya kuliwania taji la Redds Miss Tanzania linalotarajiwa kufanyika Novemba 3, mwaka huu.
 Mrembo mwingine anayetarajiwa kuingia hatua hiyo atapatikana Jumamosi katika ‘Usiku wa Redd’s Miss Tanzania’ mjini Arusha pale kutakapokuwa n akinyang’ayiro cha Miss Top Model.
 Shindano la Redd’s Miss Tanzania kwasasa linadhaminiwa n akinywaji cha Redd’s Original kinachozalishwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).

No comments