LIGI KUU YAINGIA RAUNDI YA SITA
![]() |
Ofisa Habari TFF, Boniface Wambura |
Michuano
ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwan wa Tanzania Bara inaingia raundi
ya sita wikiendi hii kwa mechi saba. Kesho (Oktoba 6 mwaka huu) African Lyon
itakuwa mwenyeji wa Azam katika mechi itakayochezwa Uwanja wa Azam Complex, Dar
es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni.
Nayo
Ruvu Shooting itaikaribisha Coastal Union ya Tanga katika mechi
itakayochezeshwa na Oden Mbaga wa Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Mabatini
ulioko Mlandizi mkoani Pwani. Mbaga atasaidiwa na Samuel Mpenzu, Ferdinand
Chacha na Andrew Shamba.
Jumapili
(Oktoba 7 mwaka huu) kutakuwa na mechi kati ya Simba na Oljoro JKT
itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Kagera Sugar na Yanga (Uwanja wa
Kaitaba mjini Bukoba), Mgambo Shooting na Polisi Morogoro (Uwanja wa Mkwakwani
jijini Tanga), Toto Africans na JKT Ruvu (Uwanja wa Kirumba jijini Mwanza) na
Tanzania Prisons na Mtibwa Sugar (Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini
Mbeya).
No comments