Ligi Kuu kuendelea kesho
Affiliated to FIFA, CAF and CECAFA
Karume Memorial Stadium, Uhuru/Shaurimoyo Road
P.O. Box 1574, Dar es
Salaam, Tanzania . Telefax: + 255-22-2861815
Release No. 167
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Oktoba 12, 2012
VPL KUENDELEA
KUTIMUA VUMBI KESHO
Michuano
ya Ligi Kuu ya Vodacom inaendelea kesho (Oktoba 13 mwaka huu) kwa timu kumi
kupambana kwenye viwanja vitano tofauti katika raundi ya saba ya ligi hiyo
yenye timu 14.
Polisi
Morogoro itaikaribisha Azam kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro wakati
mwamuzi wa FIFA, Oden Mbaga atakuwa Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini
Mbeya kuchezesha mechi kati ya wenyeji Tanzania Prisons na Oljoro JKT.
Jijini
Tanga, Simba itakuwa mgeni wa Coastal Union kwenye Uwanja wa Mkwakwani katika
mechi itakayochezeshwa na mwamuzi Simon Mberwa kutoka Pwani akisaidiwa na
Godfrey Kihwili na Abdallah Uhako wote kutoka Arusha.
Mechi
nyingine za kesho ni Ruvu Shooting dhidi ya African Lyon kwenye Uwanja wa
Mabatini mjini Mlandizi, na Mtibwa Sugar watacheza na Mgambo Shooting kwenye
Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro.
Wakati
huo huo, Azam imeomba mechi zake za nyumbani dhidi ya Yanga na Simba zichezwe
kwenye uwanja wake wa Azam Complex ulioko Chamazi badala ya Uwanja wa Taifa.
Nayo
Ruvu Shooting imeomba mechi yake ya ugenini dhidi ya Yanga ya Oktoba 20 mwaka
huu ichezwe Uwanja wa Taifa badala ya Uwanja wa Azam Complex.
Maombi
hayo yatawasilishwa kwenye kikao cha Kamati ya Ligi ya TFF kinachotarajiwa
kufanyika kesho (Oktoba 13 mwaka huu) kwa ajili ya kufanyiwa uamuzi.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
No comments