Kagera Sugar yabanwa na JKT Ruvu
Mwandishi
Wetu, Bukoba
Kagera Sugar na JKT Ruvu, leo zimetoka suluhu, katika mechi ya Ligi
Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, iliyopigwa kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, Kagera.
Pamoja na shangwe za kuichapa Yanga
kutawala uwanjani hapo, walishindwa kabisa kuzitikisa nyavu za maafande wa JKT
Ruvu.
Kwa matokeo hayo, timu hizo
zimegawana pointi moja moja, lakini JKT ikinufaika kwa kupanda nafasa moja
katika msimamo wa ligi hiyo, hivyo kuwa ya 12, huku Kagera wakiwa na point
inane.
Ligi hiyo, itaendelea kesho kwa
mchezo mmoja, utakaopigwa Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza baina ya wenyeji Toto
African na Yanga SC.
No comments