Juventus wapata tajiri wa kumsajili Drogba
JUVENTUS, Italia
KLABU ya soka ya Juventus ya Italia, imeanza mikakati ya kutaka
kumsajili mshambuliaji wa zamani wa Chelsea, Didier Drogba.
Tuttosport limesema kuwa, Juve itaweka nguvu zake kumsajili Drogba, ambaye
kwa sasa anaichezea klabu ya Shanghai Shenhua ya nchini China.
Mkurugenzi wa Juve na Kocha Antonio
Conte, walikutana baada ya mechi yao dhidi ya Siena na kujadiliana usajili wa mshambuliaji, na
kukubaliana kumrejesha mpachika mabao Drogba, barani Ulaya.
Juve, pia inasaidiwa na mfadhili
kuhakikisha mpango huo unakamilika na wanaangalia uwezekano wa kumshawishi
mcheka na nyavu huyo kutoka Ivory Coast, kwenda mjini Turin.
No comments