JOKATE AZINDUA CHAPA YA KIDOTI NA KUIBUKA NA KAULI MBIU YA ‘AINISHA UZURI WAKO’
Na Mwandishi Wetu
Miss
Tanzania namba mbili mwaka 2006, Jokate Mwegelo, amezindua rasmi lebo yake ya
mitindo ya nywele na nguo ijulikanayo kwa jina la Kidoti Brand.
Jokate ambaye alianza kujihusisha na masuala ya mitindo mwaka
jana, alizindua lebo yake hiyo kwenye hotel ya Serena na kuhudhuriwa na wadau
mbali mbali wa masuala ya urembo, maonyesho ya mavazi, wanamitindo na wauzaji
wa bidhaa hizo kutoka kila kona ya jiji.
Alisema kuwa hatua ya kuamua kuanzisha lebo hiyo ni moja ya
mikakati yake ya kujitafutia fedha kama mjasiliamali na lengo lake kubwa ni
kutaka kusimama yeye mwenyewe katika maisha bila ya kumtegemea mtu.
Alifafanua kuwa kabla ya kuanzisha lebo na kampuni yake,
alifanya utafiti wa hali ya juu, kuhusiana na sekta hiyo na hatimaye kushiriki
kwa mara ya kwanza katika maonyesho ya mavazi ya Red Ribbon na sasa kuamua
kwenda mbali zaidi kwa kuingia katika fani ya nywele ambazo anatengeneza
yeye mwenyewe.
Amesema kuwa mbali ya kushiriki katika maonyesho mbali mbali,
pia atakuwa anasambaza bidhaa zake za nywele na nguo kwenye maduka mbali mbali
ili kuwawezesha wananchi kutumia bidhaa zake.
“Lengo langu kubwa ni kutawala soko
na kuwa milionea, hiyo ndiyo ndoto yangu pamoja na kuuza bidhaa zangu hasa za
nywele kuanzia shs 9,500 na 12,000. Nguo za Kidoti zitatambulishwa rasmi katika
soko mwakani (2013) zikifuatiwa na vifuasi vya urembo pamoja na vipodozi,”
alisema Jokate.
Alisema kuwa msingi wa ubunifu wake ni mchanganyiko wa
kipekee wa kiini cha utamaduni wa Kiafrika pamoja na mitindo ya kisasa
ulimwenguni kwa ajili ya wanawake na wanaume wa kisasa.

Afisa
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Kidoti Jokate Mwegelo akizungumza wakati
alipozindua rasmi kampuni hiyo inayojishughulisha na Uuzaji wa Nywele za
Style mbalimbali Ubunifu wa mavazi ambapo ameongeza kuwa nywele hizo
zimejaribiwa na kukidhi matakwa ya kudumu, kuweza kutumiwa tena na tena,
uzito pamoja na msokotano na zitakuwa zikipatikana katika mitindo na
urefu mbalimbali zitazotumiwa na wasichana na kinamama.
Ameongeza kuwa Nywele hizo pia zitawafikia watu wa mikoani pia. Picha zote na dewjiblog.com
Afisa
Mkuu Mtendaji wa Kidoti Jokate Mwegelo akitambulisha timu ya watu
anaofanya nao kazi katika Kampuni yake kwa waandishi wa habari na wageni
waalikwa.
Pichani Juu na Chini ni Models wakionyesha aina tofauti za Nywele za Kidoti zinazotengenezwa na Darling Tanzania.
Selita Style.
Hii ni aina ya Nywele inayoitwa Jokate,
Aina ya Nayomi.
Models katika picha ya pamoja mbele ya wageni waalikwa.
Meneja
Masoko wa Kampuni ya Kidoti Peter Kasiga akielezea ubora wa Nywele hizo
na bei zake kwa wageni waalikwa na wandishi wa habari waliohudhuria
uzinduzi huo leo jijini Dar es Salaam.
Meneja
Masoko wa Kampuni ya Kidoti Peter Kasiga pamoja na CEO wa Kidoti Jokate
Mwegelo wakijibu maswali kwa waandishi wa habari wakati wa uzinduzi huo
ambapo pia amefafanua kuzinduliwa rasmi kwa tovuti ya kampuni hiyo leo
itakayopatikana kupitia anuani ya www.kidotiloving.com
CEO wa Kidoti Jokate Mwegelo katika picha ya pamoja na Models waliovaa nywele za Sanisi za Kidoti.
CEO
wa Kidoti Jokate Mwegelo katika picha ya pamoja na timu ya wafanyakazi
wa kampuni yake. Kushoto ni Meneja Masoko Bw. Peter Kasiga, Operation
Manager wa Faith Lukindo (katikati), Meneja Biashara Bruce Paschal (wa
pili kushoto) na Meneja Mauzo Charles Benson.
“Ainisha Urembo Wako” by Jokate Mwegelo.
Pichani
Juu na Chini ni Baadhi ya wageni waalikwa na wadau wa tasini ya urembo
waliohudhuria uzinduzi huo uliofanyika jijini Dar es Salaam leo katika
Hoteli ya Serena.
CEO wa Kidoti Jokate Mwegelo akiwa na mbunifu nguli wa mavazi Khadija Mwanamboka a.k.a Kubwa la maadui.
Jokate Mwegelo akimpiga busu Khadija Mwanamboka kama ishara ya kumushukuru baada ya kuhudhuria uzinduzi wa kampuni yake.
CEO
wa Kidoti Jokate Mwegelo katika picha ya pamoja baadhi ya marafiki
waliojumuika naye katika uzinduzi wake. Katikati ni Mdau Calvin na
Fashionista Bella all the way from UK.
Jokate Mwegelo akishow love na Binamu yake Esi Sebastian na Mdau William Maelecela a.k.a Lemutuz.
Jokate Mwegelo na Cousin Sister wake Esi Sebastian.
CEO
wa Kidoti Jokate Mwegelo akiwa na mmoja wa mawakala wake Said Rundika
mwenye duka la Jumla Kariakoo mkabala na kituo cha Mafuta cha Big Bon
eneo la Msimbazi.
Jokate Mwegelo na rafiki yake kipenzi Bella.
No comments