JKT Oljoro, Coastal Union zatoshana nguvu
JKT Oljoro, ilishindwa kuutumia vizuri uwanja
wake wa nyumbani wa Sheikh Amri Abeid Karuta, baada ya kutoka sare ya mabao 2-2
dhidi ya Coastal Union, katika mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara.
Coastal Union walikuwa wa kwanza kupata bao
lililofungwa na Kassim Selembe, dakika ya 35, baada ya kuwatoka mabeki wa
Oljoro JKT na kupiga shuti kali lililokwenda moja kwa moja wavuni.
Kipindi cha pili JKT Oljoro walikianza kwa kasi na
kulifikia lango la wapinzani, ambapo dakika ya 50, Paul Nonga, aliisawazishia
timu yake bao, kufuatia uzembe wa mabeki wa Coastal Union wakifikiria kuwa,
ameotea.
Bao hilo liliwaongezea nguvu JKT Oljoro, ambapo
dakika ya 60, walifanikiwa kupata bao la pili lililofungwa na Meshack Nyambere,
baada ya kuwatoka mabeki wa Coastal Union na kuukwamisha mpira wavuni.
Coastal Union, walikuwa ving’ang’anizi na kuwabana
wenyeji wao, ambapo dakika ya 77, Said Sued aliisawazisha timu hiyo bao la pili
lililowafanya wagawane pointi.
No comments