Chelsea FC yazidi kutakata England
![]() |
Juan Mata |
LONDON, England
MABAO mawili ya kiungo Juan Mata, yamekisaidia
kikosi chake cha Chelsea kuibuka na ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya mahasimu wao
wa London, Tottenham Hotspur, katika mchezo wa Ligi Kuu ya England ,uliochezwa kwenye
wa White Hart Lane, leo.
Chelsea wameendeleza rekodi yao ya
kutopoteza mchezo, ambapo bao lao la kwanza liliwekwa nyavuni na beki Gary
Cahill.
Tottenham walisawazisha baada ya
mapumziko, bao hilo likifungwa na beki William Gallas, kabla ya Jermain Defoe,
kufunga bao la kuongoza.
Hilo lilikuwa bao la 200 la Defoe
katika kipindi chake cha soka, lakini halikutosha kumpa kocha wa Spurs, Andre
Villas Boas
ushindi, dhidi ya klabu ambayo ilimtimua Machi mwaka huu, baada ya Mata
kusawazisha.
Baadaye nyota huyo wa Hispania,
alipachika bao lingine na kumwacha kipa wa Spurs, Brad Friedel,
akichanganyikiwa.
Kabla ya Tottenham kusawazisha, Daniel
Sturridge, aliiongezea Chelsea bao la nne, dakika za nyongeza.
Kikosi hicho cha Roberto Di Matteo, ambao
ni mabingwa wa Ulaya, kina pointi 22, baada ya mechi nane.
No comments