BREAKING NEWS; JESHI LAINGIA MITAANI KUDHIBITI HALI YA USALAMA DAR ES SALAAM
Muumini wa dini ya Kiislamu akishahadia kwa mola wake na kusema nipo tayari kufa kwa ajili ya kutetea dini ya Allah baada kukamatwa na Askari wa Kikosi cha Kutulia Ghasia katika viunga vya Ikulu leo. (Picha zote na Happiness Mnale)
Askari wa Kikosi cha kutuliza Ghasia (FFU) wakijiandaa kumwingiza katika
gari muumini wa Kiislamu aliyekamatwa katika maeneo ya Ikulu
Barabara ya kuingia katika Ofisi za Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
zikiwa zimefungwa na Askari Polisi kufuatia vurugu zilizotokea leoPolisi wakifanya doria kwa kutumia pikipiki
Mitaa ya Kariakoo na viunga vyake ikiwa imeimarishwa na Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika mitaa ya Kariakoo leo
Ulinzi uliimarishwa na Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania katika mitaa ya Kariakoo leo
Wanajeshi wakivinjari katika mitaa ya Kariakoo leo
Askari wa jiji wakishiriki kikamilifu katika zoezi la kuwakamata watu waliokuwa wamekusanyika kwa nia ya kutaka kuandamana katika eneo la Kariakoo
Magari ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania yakiwa katika doria katika barabara ya Msimbazi ambako kulitokea vurugu zilizosababishwa na waislamu waliotaka kuandamana.
Dar es Salaam, Tanzania
Watu hao walifika mmoja mmoja maeneo ya Ikulu kabla ya kudhibitiwa na Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) na kupelekwa Kituo Kikuu cha Kati.
Kukamatwa kwa watu hao kunafuatia Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kuwatawanya waumini wa dini ya Kiislamu ambao walikuwa na nia ya kufanya maandamano.
Waandishi wameshuhudia gari mbili za jeshi la Polisi zikiwa zimebeba wanajeshi waliokuwa na silaha.
Katika maeneo ya Kariakoo vikosi vya Jeshi la wananchi wa Tanzania vimekuwa vikifanya doria ili kuimarisha hali ya ulinzi.
No comments