Header Ads

ad

Breaking News

BARCELONA, MADRID HAKUNA MBABE NOU CAMP, INTER KIJOGOO


BARCELONA, Hispania
LIONEL Messi na Mreno Cristiano Ronaldo, Jumapili Oktoba 7, walionesha ubora wao katika soka, baada ya kila mmoja kuifungia timu yake mabao 2-2, wakati miamba ya soka Barcelona na Real Madrid, ilipokutana uwanjani katika mechi ya ligi kuu Hispania.
Mechi hiyo iliyopigwa Nou Camp jijini Barcelona, iilianza kushuhudia nyavu zikitishwa na Mreno, Cristiano Ronaldo dakika ya 23, huku Messi akisawazishabao hilo dakika ya 31.
Mechi hiyo kubwa ilihudhuriwa na mashabiki 95,000, liliwashuhudia miamba hao wa Hispania wakienda mapumziko wakiwa wamefungana bao 1-1.
Mchezaji bora wa Dunia na Ulaya, Messi aliifungia Barcelona bao la pili dakika ya 61, lakini Ronaldo alifanya kama alivyofanya Messi awali, kwa kuifungia bao la kusawazisha bao hilo dakika tano baadaye na kumaliza pambano hilo la 222 baina ya klabu hizo kwa sare ya 47 katika historia yao, ambapo Madrid imeshinda mara 88 na Barca mara 87.
Mechi nyingine kubwa wikiendi hii ilikuwa nchini Italia, Inter Milan ilishinda bao 1-0 dhidi ya AC Milan, kwenye Uwanja wa San Siro.

No comments