Header Ads

ad

Breaking News

Azam FC yaisogelea Simba Ligi Kuu Bara



Azam FC

Na Mwandishi Wetu, Morogoro

TIMU ya Azam FC ya jijini Dar es Salaam, jana iliendeleza wimbi la ushindi baada ya kuilaza Polisi Morogoro bao 1-0, katika mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

Katika mchezo huo ulioanza kwa timu zote kusomana mchezo, kila timu ilikuwa ikisaka bao la mapenzi ili iweze kujihakikishia kuibuka na ushindi katika uwanja huo.

Hata hiovyo, wageni Azam FC, ndio waliofanikiwa kupata bao hilo dakika ya 36, lililofungwa na Kipre Tchetche, akitumia vizuri mpira uliopanguliwa na  kipa wa Polisi Moro, Manzi Manzi uliopigwa na John Bocco.

Tchetche aliunasa mpira uliokuwa ukichezewa na  kipa huyo, kabla ya kuzipasia nyavu mpira huo na kuwa bao pekee katika mchezo huo.

Dakika ya 90, Polisi Moro walipata nafasi nzuri ya kusawazisha bao hilo, lakini Malimi Basungu, akiwa peke yake alishindwa kuisawazishia timu yake bao hilo.

Kwa matokeo hayo, Azam imefikisha pointi 16, ikizidia pointi moja na Simba, ambao ni vinara wa ligi hiyo.
Kutoka katika Uwanja wa Mabatini Mlandizi, Pwani, Mwandishi Wetu anaripoti kuwa, wenyeji Ruvu Shooting, jana waliibuka na ushindi wa bao 1-0, dhidi ya African Lyon ya jijini Dar es Salaam.

Ruvu Shooting ilianza mchezo kwa kulisaka lango la African Lyon, ambapo dakika ya tano, Ayoub Kitala, alipiga shuti kali, lakini kipa wa Lyon Abdurhaman Mussa aliudaka mpira huo.

Dakika ya nane, Hood Mayanja, alifanya shambulizi la nguvu, lakini mpira uliokolewa na Mangasin Mbonosi.
Ruvu Shooting walijipatia bao dakika ya 45, lililofungwa na Raphael Keyala, akitumia vizuri krosi iliyopigwa na Mussa na kuujaza mpira wavuni.

Katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine, Mbeya, Mwandishi Wetu anaripoti kuwa, maafande wa Oljoro JKT, jana waligoma kutumbukizwa gerezani na maafande wa Prisons, baada ya kuwachapa bao 1-0.

Bao la washindi lilipatikana dakika ya tano, kupitia kwa Amir Omary, na kuufanya mchezo huo kuwa wa kasi, huku Tanzania Prisons wakitafuta bao la kusawazisha.

No comments