13 WAPITISHWA KUGOMBEA UONGOZI TWFA
Wagombea
13 kati ya 15 waliojitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi kwenye Chama
cha Mpira wa Miguu wa Wanawake Tanzania (TWFA) wamepitishwa baada ya usaili
uliofanyika juzi.
Kwa
mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TWFA, Ombeni Zavala,
waliopitishwa kwenye nafasi ya uenyekiti ni Isabellah Huseein Kapera, Joan
Ndaambuyo Minja na Lina Paul Kessy.
Makamu
Mwenyekiti ni Rose Kisiwa wakati wanaowania nafasi ya Katibu Mkuu ni Amina Ali
Karuma na Cecilia Oreste Makafu. Mgombea pekee wa nafasi ya Katibu Msaidizi,
Macky Righton Mhango naye amepita kwenye usaili huo. Aliyepitishwa kwenye
nafasi ya Mhazini ni Rose Stewart Msamila.
Furaha
Francis na Zena Chande wamepitishwa kuwania nafasi ya Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) wakati waliopita kuwania ujumbe wa
Kamati ya Utendaji ya TWFA ni Triphonia Ludovick Temba, Rahim Salum Maguza na
Sophia James Charles.
Hivi
mchakato wa uchaguzi wa TWFA uko katika kipindi cha kukata rufani ambapo ni
kuanzia Oktoba 15-17 mwaka huu. Rufani zinatakiwa zifike kwa Katibu Mkuu wa TFF
kabla ya saa 10 kamili jioni ya Oktoba 17 mwaka huu.
Wagombea
wawili ambao hawakupitishwa kwa ajili ya uchaguzi huo
unaotarajiwa
kufanyika Novemba 4 mwaka huu ni Julliet Mndeme na Jasmin Soud walioomba ujumbe
wa Mkutano Mkuu wa TFF. Wagombea hao ambao pia walikuwa wamewekewa pingamizi
hawakufika kwenye usaili.
No comments