Viongozi wa afrika washirikiana na viongozi wa dunia kusukuma ukuaji wa kilimo katika Afrika
(Melinda
Gates, Rais Jakaya Kikwete wa Tananzia na Kofi Annan kwenye mkutano wa
Mageuzi ya Kilimo cha Afrika mjini Arusha Tanzania)
……………………………………………………………………………………………………………….
Mkutano wa Mageuzi ya Kilimo cha Afrika waanza mjini Arusha Tanzania
“Tuna mwelekeo wa kuweza kupata
ufanisi katika juhudi zetu za kuangamiza njaa na umaskini katika Afrika,
kupitia njia ya mageuzi ya kilimo.”alisema Rais Kikwete. “Kwa
mchanganyiko wa maongozi bora, kuchukuliwa kwa maamuzi sawa na serikali
za mataifa yetu ya Afrika, uendelevu wa misaada kutoka kwa wafadhili na
kushiriki kikamilifu kwa sekta ya kibinafsi katika nchi zetu na
kwingineko kadhalika, mageuzi ya kilimo cha Afrika yanaweza kufikiwa.”
Akifungua mkutano huo, Kofi Annan,
Mwenyekiti wa Umoja wa Mageuzi ya Kilimo cha Afrika – Alliance for a
Green Revolution in Africa (AGRA) alieleza juu ya ufanisi uliofikiwa
tangu mkutano wa kwanza wa AGRF mnamo mwaka wa 2010. Bw. Annan pia
alisisitiza juu ya umuhimu wa kuwaboresha wakulima wa mashamba madogo
kwa kuwasaidia kwenda mbele kupelekea mazingira ya kilimo cha biashara.
“Lengo letu la kuongeza
uzalishaji na faida kwa wakulima wa mashamba madogo – wengi wao wakiwa
ni wanawake – haliwezi kuyumba. Wao ndio wanaotuwekea chakula kwenye
meza zetu, Wao ndio wanaotunza rasilamali zetu za ardhi na maji” alisema
Bw. Annan. Hatimaye, wao ndio watakao sukuma ukuaji wa uchumi na
maendeleo ya Afrika katika karne ya 21.”
Melinda Gates, Mwenyekiti
mshiriki wa Wakfu wa Bill & Melinda Gates, ambaye alikwenda Arusha
kuhutubia wajumbe wa mkutano huu, alitambua maendeleo makubwa ya kilimo
cha Afrika yaliyofikiwa ndani ya muda wa muongo mmoja uliopita, na
akatoa wito kwa viongozi wa Afrika waendelee kuunga mkono juhudi hizo.
“Nawahimiza viongozi wa Afrika
kuzingatia upya ahadi zenu za kuongeza uzalishaji wa jamii ya wakulima.
Nawahimiza kuweka ajenda ya muongo ujao, itakayokuwa na ari kubwa
zaidi,” alisema Bi. Gates. “Natumai mtakuwa makini kweli kuhakikisha
kwamba ahadi na mipango yenu itapelekea kuwasaidia jamii za wakulima
hawa kufikia malengo yao.”
No comments