TWFA YATANGAZA KAMATI YA UCHAGUZI
Lloyd Nchunga |
Chama
cha Mpira wa Miguu wa Wanawake Tanzania (TWFA) kimetangaza Kamati ya Uchaguzi
yenye wajumbe watano kwa ajili ya uchaguzi wake unaotarajiwa kufanyika Novemba
mwaka huu.
Kaimu
Mwenyekiti wa TWFA, Margreth Mtaki amewaambia Waandishi wa Habari, Dar es
Salaam leo kuwa kamati hiyo itaongozwa na Ombeni Zavala, na itarajia kutangaza
mchakato wa uchaguzi huo Jumatatu (Septemba 24 mwaka huu).
Aliwataja
wajumbe wengine wa kamati hiyo yenye jukumu la kuendesha uchaguzi wa chama
hicho kuwa ni Rachel Masamu, Lloyd Nchunga, Nancy Mabula na Maneno Tamba.
Pia
aliwataka wadau wa mpira wa miguu wa wanawake kujitokeza kugombea nafasi
mbalimbali za uongozi katika TWFA mara Kamati ya Uchaguzi itakapoanza mchakato.
Wakati
huo huo,
uchaguzi wa vyama vya mpira wa miguu vya mikoa ya Kilimanjaro (KRFA) na Manyara
(MARFA) unafanyika kesho (Septemba 22 mwaka huu).
No comments