Thadeo mgeni rasmi pool Taifa
Na
Mwandishi wetu,Mwanza
MKURUGENZI wa Michezo
wa Wizara ya Habari, Utamaduni , Vijana na Michezo, Leonard Thadeo, kesho
anatarajia kuwa mgeni rasmi katika kilele cha fainali za taifa za mashindano ya
pool ya Safari Lager (Safari Lager National Pool Championship 2012).
Mashindano
hayo yanayodhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) ,kupitia bia yake ya
Safari Lager, zitafanyikia kwenye ukumbi wa hoteli ya Monarch iliyopo mkoani Mwanza,
ambapo timu za Meeda ya Kinondoni na Kayumba ya Ilala zote kutoka Dar es Salaam,
zikiwania ubingwa huo.
Meeda
ilifanikiwa kutinga hatua ya fainali baada ya kuichapa Anatory ya Morogoro mabao13-10
katika hatua ya nusu fainali, huku Kayumba ikiichapa 2eyes ya Arusha mabao 13-9,
katika mchezo wa nusu fainali.
Kwa
upande wa mchezaji mmoja mmoja (wanaume), Solomon Elias kutoka Mbeya, alikuwa
wa kwanza kutinga fainali, baada ya kumfunga Ally Nada wa Manyara mabao 4-0, hivyo kumsubiri mshindi kati ya Fayuu Stanley
wa Arusha na Athuman Seleman wa Morogoro kwa ajili ya kucheza fainali.
Kwa
upande wa mchezaji mmoja mmoja (wanawake), Cesilia Kileo wa Kilimanjaro na
Betty Sanga wa Mbeya, watachuana katika hatua ya fainali, baada ya kushinda
michezo yao ya nusu fainali.
Cecilia
alimtoa Sada Tulla wa Shinyanga mabao 4-3, wakati Betty alitingahatua hiyo kwa
kumfunga Anna Peter wa Iringa mabao 4-0.
Bingwa
kwa upande wa timu ataondoka na fedha taslim sh.milioni tano, kombe na medali za dhahabu, wakati bingwa kwa
upande wa mchezaji mmoja mmoja (wanaume), atajizolea sh.500,000 na bingwa wa
mchezaji mmoja mmoja (wanawake), atazawadiwa sh.350,000.
Mbali
ya zawadi kwa washindi hao, lakini kuanzia mshindi wa pili kwa upande wa timu
hadi wa mwisho, kila moja itaondoka na zawadi za fedha taslim kulingana na nafasi,
huku zawadi hizo zikienda pia kwa mchezaji mmoja mmoja wanaume na wanawake.
No comments