TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
KILIMANJARO LAGER YAKABIDHI MABASI KWA SIMBA
NA YANGA
Septemba 21, 2012-Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia bia
yake ya Kilimanjaro Premium Lager leo imetoa mabasi mawili kwa klabu za Simba
na Yanga. Mabasi hayo ya kifahari yana thamani zaidi ya Sh milioni 450.
Hafla ya makabidhiano hayo imefanyika
Makao Makuu ya TBL, mbele ya Mkurugenzi Mkuu wa TBL, Robin Goetzsche pamoja na
makundi ya Simba na Yanga pamoja, wadau mbalimbali wa mpira wakiwemo pia
waandishi wa habari. Kununuliwa kwa mabasi hayo kumefanywa na TBL kwa mujibu wa
mkataba baina yake na klabu hizo kubwa nchini.
Akizungumza katika hafla hiyo,
Mkurugenzi Mkuu alisema: “Tunaona heshima kubwa sana kuwa na uhusiano na klabu
hizi ambazo daima zina mafanikio.
“Malengo yetu ni kukuza soka nchini Tanzania
na kwa kuanzia tumeona tushirikiane na Simba na Yanga ambazo kila zinapokutana
uwanjani hali huwa ya kuchangamka sana katika mwendelezo wa Ligi Kuu.”
Alisema mabasi hayo yaliyotolewa
kwa klabu hizo, yalenge kuinua soka na kuzitaka klabu hizo kuyatunza mabasi
hayo kwa maslahi ya wachezaji na watendaji wengine. “Tutaendelea kuwapa msaada
pale kwa vile tunatarajia kuwa mtaleta faida kwa maana ya matokeo mazuri katika
soka kwa kutwaa mataji na kama wengi tujuavyo, mpira ni mabao.”
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro
Premium Lager, George Kavishe alisema mabasi hayo yenye uwezo wa kubeba watu 51
yamenunuliwa kutoka Yutong.
Alisema mabasi hayo ni ya kisasa kabisa kwani yanabeba abiria 51 akiwemo dereva, ni
imara kwani chasis yake ni 4x2, injini ya mabasi haya ni aina ya 300 HP Cummins,
yana retarder ya umeme and breki aina ya
ABS, yana TV mbili za kisasa, muziki wa nguvu wenye spika nane, milango na
mabuti ya kisasa, kioo cha kuangalia nyuma kinachotumia umeme, jokofu na kiyoyozi.
“Tunataka wachezaji wetu wawe na
raha wanaposafiri. Hii ndiyo maana tumeamua kutoa mabasi haya ya kifahari
ambayo ndani yake kuna huduma muhimu kama televisheni, friji, vitu ambavyo
tunaamini mtavitunza.”
Aliongeza kuwa pamoja na ukweli
kwamba TBL inawajibika kununua mabasi hayo kwa mujibu wa mkataba, lakini lengo
kuu ni kuona kuwa wachezaji wanakuwa katika mazingira mazuri.
Baada ya makabidhiano hayo, wahudhuriaji
kutoka klabu hizo walicheza na kufurahia mabasi hayo huku wakiimba nyimbo
mbalimbali.
Bia ya Kilimanjaro ilianza
kuzidhamini Simba na Yanga tangu mwaka 2008.
Kwa maelezo zaidi:
George
Kavishe, TBL, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, +255 767 266786, George.Kavishe@tz.sabmiller.com
Michael
Mukunza, Executive Solutions Limited, +255 776 978302, m.mukunza@executivesolutionstz.com
No comments