Header Ads

ad

Breaking News

ST8MUZIK Freestyle 2012 ilivyotikisa Mwanza


Mshindi wa mpambano wa maDj wa ST8MUZIK Freestyle 2012 mkoani mwanza DJ Juma Ramadhani(Kati) akitumbuiza mara baada ya kukabidhiwa chombo cha kupigisha muziki chenye thamani ya sh mil. 7 na Meneja wa TCC Mkoa wa Mwanza, Deogratius Kamugisha (kulia), huku mshindi wa upande wa MC mkoani humo, Joash Magadula, akishuhudia akiwa na zawadi yake mkononi.



Meneja wa TCC Mkoani Mwanza Deogratius Kamugisha, akimkabidhi tuzo MC bora wa ST8MUZIK Freestyle 2012 mkoani Mwanza, Joash Magadula, katika mchuano uliofanyika katika ukumbi wa Stone mjini Mwanza, juzi.



Meneja wa TCC tawi la Mwanza, Bw Deogratius Kamugisha (Katikati) akipozi na washindi wa mpambano wa ma MCs na DJs STR8MUZIK Freetyle 2012 mkoani mwanza. Kutoka kushoto ni Mshindi wa pili wa DJs Ruyobya Johannes a.k.a DJ Yt,Mshindi wa kwanza kwa DJs Juma Ramadhani, msindi wa pili katika kategori ya MC, Nchana Antony na Mshindi wa MC Joash Magadula ‘ MC Magadash’. (Picha zote na Executive Solutions)



Umati wa wana Mwanza ulivyojaa katika ukumbi Club Stone mjini humo, katika mpambano wa STR8MUZIK 2012 FreeStyle Mwanza.



Mmoja wa wasanii waliotoa burudani, akifanya mambo yake mbele ya umati wa mashabiki wa burudani jijini Mwanza, wakati wa shindano la STR8MUZIK 2012 FreeStyle lililofanyika katika ukumbi Club Stone mjini Mwanza, juzi.

No comments