SHUKRANI KWA WADAU SERENGETI BOYS
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linawashukuru wadau waliofanikisha kwa njia
mbalimbali ziara ya timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17
(Serengeti Boys) iliyofanyika hivi karibuni katika mikoa ya Mbeya na Njombe.
Wadau
hao ni Chama cha Mpira wa Miguu Mbeya Mjini (MUFA) chini ya Mwenyekiti wake
Suleiman Haroub, Kaimu Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Njombe
(NJOREFA), Stanley Lugenge, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mbeya (MREFA) na
Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Njombe (NDFA).
Wengine
ni Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Makambako (MDFA), Chama cha Mpira wa
Miguu Mkoa wa Morogoro (MRFA), na klabu za Mbozi United, Kyela United, Tanzania
Prisons na Mbeya City.
Serengeti
Boys inaendelea na kambi yake jijini Dar es Salaam kujiandaa kwa mechi ya
kwanza ya mchujo ya michuano ya Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17
dhidi ya Misri itakayochezwa Oktoba 14 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
No comments