Serengeti Boys kujipima kwa Ashanti United
Timu ya Taifa ya vijana wenye umri
chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) baada ya ziara ya Mbeya imerejea Dar es
Salaam ambapo inaendelea na maandalizi na kesho (Septemba 26 mwaka huu)
itacheza mechi ya kirafiki na timu ya daraja la kwanza ya Ashanti United.
Mechi hiyo itachezwa Uwanja wa
Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam kuanzia saa 10 jioni kwa kiingilio cha sh.
500 tu.

No comments