RAIS KIKWETE AOMBOLEZA KIFO CHA MKURUGENZI MKUU WA KWANZA WA TAKUKURU, MEJA JENERALI (mstaafu) ANATOLI KAMAZIMA 2
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini katika kitabu cha
maombolezo nyumbani kwa Marehemu Meja jenerali Kamazima Tegeta, Dar es salaam,
leo.
Rais na Amiri Jeshi Mkuu Dkt Jakaya Mrisho
Kikwete akitoa pole kwa mjane na ndugu wa wa Meja Jenerali Mstaafu
Anatoli Kamazima leo nyumbani kwa marehemu Tegeta, Dar es salaam.
Marehemu Kamazima, ambaye amefariki dunia usiku wa kuamkia
leo Jumatano ya Tarehe 26 Septemba, 2012 utokana na mshtuko wa moyo,
alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa kwanza wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
nchini TAKUKURU.
Rais na Amiri Jeshi Mkuu Dkt Jakaya Mrisho
Kikwete akiongea na Brigedia Jenerali Mstaafu Tindamanyire, ndugu wa
hayati Meja Jenerali Mstaafu Anatoli Kamazima, leo
nyumbani kwa marehemu Tegeta, Dar es salaam. Kulia kwa Rais ni Mkuu wa
Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange na Mnadhimu Mkuu Luteni Jenerali Samwel
Albert Ndomba. Marehemu Kamazima, ambaye amefariki dunia usiku wa kuamkia
leo Jumatano ya Tarehe 26 Septemba, 2012 utokana na mshtuko wa moyo,
alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa kwanza wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
nchini TAKUKURU.
No comments