Papic aishtaki Yanga FIFA
![]() |
Kostadin Papic |
Tumepokea
barua kutoka Kitengo cha Sheria cha Shirikisho la Kimataifa la Vyama vya
Mpirawa Miguu (FIFA) likitutaka tuitaarifu Yanga kuhusu mashtaka
yaliyowasilishwa na kocha wazamani wa klabu ya Yanga, Kostadin Papic.
Katika malalamiko yake, Papic anadai kuwa
hajalipwa malimbikizo ya mshahara wake yanayofikia kiasi cha Dola 12,300 za
Kimarekani. Katika barua yake, kocha huyo anadai kuwa alikuwa akiwasiliana na
maofisa na viongozi waYanga, lakini hakupata ushirikiano na hivyo kuamua kwenda
FIFA. TFF ilifanya juhudi za kuwasiliana na Yanga kuhusu malalamiko hayo ili
kujaribu kumzuia kocha huyo asishtaki FIFA, lakini juhudi hizo hazikuzaa
matunda.
Kama
chombo kinachosimamia uendeshaji wa mpira wa miguu nchini, TFF imesikitishwa na
habari hizo na inaiomba klabu ya Yanga kufanya kila jitihada kuhakikisha kuwa
inawasilishataarifa zote muhimu na nyaraka zinazohusiana na stahiki za kocha
huyo ili kama ilishamalizana naye, sifa ya klabu ya Yanga isafishwe. Tayari
barua imeshaandikwa kwa klabu ya Yanga kuitaka itekeleze utashi huo mapemz
iwezekanavyo.
Tukio
hilo, si tu linachafua sifa ya klabu ya Yanga, bali soka ya Tanzania kwa ujumla
kutokana na ukweli kwamba ikishadhihirika kuwa kuna tatizo la malipo ya makocha
nchini, ni dhahiri kuwa itakuwa ni vigumu kwa klabu zetu na hata timu za taifa
kupata makocha wazuri kutoka nje kwa kuwa watakuwa wamejengeka hofu ya kufanya
kazi nchini.
Hili
ni tukio la pili kwa Yanga baada ya mchezaji wake mwingine, John Njoroge
kuishtaki klabu hiyo FIFA na kushinda kesi yake iliyoamuliwa mwezi Januari na
Kitengo cha Usuluhishi wa Migogoro cha FIFA (DRC). Ushindi wa Njoroge
unamaanisha kuwa iwapo Yanga itashindwa kutekeleza kumlipa mchezaji huyo kasi
cha Sh milioni 17, inaweza kujikuta katika adhabu ambayo itatulazimisha
tuishushe daraja; kuinyang’anya pointi kwa kiwango kitakachotajwa na FIFA;
kuipiga faini au adhabu zote kwenda kwa pamoja. Tunaiomba Yanga itekeleze
hukumu hiyo kwa wakati uliotajwa kwenye barua ya FIFA ili kuepuka hatua hizo.
Suala
la Njoroge ni moja kati ya matukio mengi yanayohusu ukiukwaji wa taratibu za
kuvunja mikataba yanayofanywa na klabu zetu. Kuna malalamiko ya wachezaji wengi
dhidi ya klabu zao za zamani kuhusu kutolipwa stahiki zao. Hivyo TFF inatoa
wito kwa klabu kujiepusha na vitendo hivyo kwa kuwa vinawanyima haki wachezaji,
lakini pia vinachafua sifa ya nchi iwapo wachezaji wanachukua hatua za kwenda
kwenye vyombo vya juu.
Tumekuwa
tukisoma kwenye vyombo vya habari kuhusu kutimuliwa kwa sekretarieti nzima ya
Yanga kutokana na kuonekana kuwa ina udhaifu. Taarifa hizo hazijaifikia rasmi
TFF. Kiutaratibu, Yanga inatakiwa iwsasilishe majina ya maofisa watakaofanya
kazi na TFF kwa sasa na itakapoajiri sekretarieti ya kudumu, basi itume barua
nyingine ya kuwatambulisha watendaji wake.
Kama
itakuwa imeitimua sekretarieti nzima, basi TFF inapokea taarifa hizo kwa
masikitiko makubwa. Si nia ya TFF kutetea watendaji wazembe, lakini klabu
hazina budi kufuatilia kwa karibu utendaji wa sekretarieti zao ili isije
ikafikia wakati sekretarieti nzima inaondolewa kwa makosa ambayo yangeweza
kusahihishwa kama kungekuwa na ufuatiliaji wa karibu.
TFF
imekuwa ikitoa mafunzo kwa watendaji wa klabu ili waweze kufanya kazi zao vizuri
na kwa mintaarafu ya mpira wa miguu na hivyo kuondolewa kwa timu nzima kama
hiyo kunamaanisha kuwa ni upotevu wa rasilimali ambayo imetumika kuwapa elimu
ya kutenda kazi zao vizuri.
TFF
ilishafanya kozi ya Event Management kwa ajili ya watendaji wa klabu; semina ya
kuangalia upya maazimio ya Bagamoyo kwa watendaji na viongozi na pia kozi ya
utawala hivyo haipendi juhudi hizi zipotee kirahisi.
No comments