MUDA WA MECHI ZA ‘LIVE’ SUPER WEEKEND
![]() |
Msemaji wa TFF, Boniface Wambura |
Mechi
tano za Ligi Kuu ya Vodacom za Super Weekend katika mzunguko wa kwanza
zitakazooneshwa moja kwa moja na kituo cha televisheni cha Super Sport zitaanza
kati ya saa 1-.30 jioni na saa 1 kamili usiku.
Septemba
28 mwaka huu kutakuwa na mechi kati ya Azam na JKT Ruvu itakayofanyika Uwanja
wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 1 kamili usiku. Mechi ya Simba na Tanzania
Prisons itakayochezwa Septemba 29 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
itaanza saa 11 kamili jioni.
Yanga
na African Lyon zenyewe zitapambana Septemba 30 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam kuanzia saa 11 kamili jioni wakati Ruvu Shooting na Mtibwa Sugar
zitaoneshana kazi Oktoba 1 mwaka huu Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam
kuanzia saa 10.30 jioni.
Mechi
ya mwisho katika Super Weekend itakuwa Oktoba 3 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam ikiwakutanisha watani wa jadi Yanga na Simba, na itaanza kutimua
vumbi saa 1 kamili usiku.
No comments