MKUTANO VODACOM, KLABU ZA LIGI KUU
Klabu
za Ligi Kuu na mdhamini wa ligi hiyo kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom
zimekutana jana (Septemba 27 mwaka huu) jijini Dar es Salaam.
Mazungumzo
yalilenga kipengele ya upekee (exclusivity) kilichopo kwenye mkataba wa
udhamini ambacho kitaendelea kuwepo. Klabu zilikuwa zimeomba kwa mdhamini
kuangalia uwezekano wa kukiondoa.
Pande
hizo zimekubaliana kuunda kamati ya pamoja kwa ajili ya kuitafutia kila klabu
mdhamini binafsi kwa lengo la kuhakikisha zinashiriki kikamilifu katika ligi
hiyo.
Klabu
zote zimeshapata vifaa kutoka kwa Vodacom ukiondoa African Lyon ambayo
ilitarajia kuchukua vifaa hivyo leo kutoka kwa mdhamini wa ligi hiyo.
No comments