MKALI RICK ROSS “TUFLON DON” KUTOKA NCHINI MAREKANI KUTIKISA SERENGETI FIESTA OKTOBA 6/2012

Akizungumza na Mtandao wa
Fullshangweblog kwa njia ya simu jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa
kamati ya Maandalizi ya Fiesta Bw. Sebastian Maganga amesema mwanamzuki
huyo atakuja nchini na kila kitu kiko sawa kwa ajili ya kufanya vitu
vyake katika tamasha la Serengeti Fiesta 2012 hapo Septemba 6 mwaka huu
jijini Dar es salaam.
Amewataka mashabiki wa Serengeti
Fiesta kuja kumshuhudia gwiji huyo wa muziki kutoka nchini Marekani
wakati atakapofanya mambo makubwa jukwaani katika tamasha hilo.
Sebastian Maganga ameongeza kwa
jukwaa la Fiesta ni jukwaa ambalo vijana wa kitanzania wanaweza
kulitumia vizuri kuonekana kimataifa kutokana na kwamba wanakuwa
wanapanda na kufanya kazi jukwaa moja na wanamuziki wa kimataifa kutoka
mataifa mbalimbali tangu tulipoanza Shangwe hizi za fiesta zaidi ya
miaka 10 iliyopita sasa
No comments